2017-03-13 15:17:00

Wapo wanawake walei wenye ari na kuonesha utajiri mkubwa wa imani


Miongoni mwa mipango mingi iliyofanyika kuienzi  Siku ya Wanawake Duniani iliyofikia kilele chake tarehe 8 Machi 2017 ,Utume wa Kanisa Katoliki huko Brisbane nchini Australia uliandaa tukio la kwa ajili ya wahudumu wake ambapo waliwasilisha historia  za wawake wamissionari kwa huduma  zao za ajabu katika jumuiya na kwa ajili ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi; watoto yatima na wale wote wanaohitaji msaada wa pekee. Baadhi ya historia hizi zilitangazwa  hata katika vyombo habari na mitandao ya  kijamii kwa njia ya utume Katoliki nchini Australia kwa kuweka  mfululizo wa matukio mbalimbali waliyo yaita “wanawake na utume”.

Mfululizo wa matukio hayo ulitolewa wiki iliyopita ukiwa unawakilisha mada ya Siku  ya wanawake duniani kwa mwaka 2017, kwa kauli mbiu  “uwe pembeni kubadilika.Wanawake wa utume  wanatoa historia za watawa na wanawake walei  kama viongozi katika utume wakishiriki kwenye elimu , afya , huduma za jamii na malezi ya kiroho katika jamii ya bara la Asia, Afrika, Amerika ya Kusini na Australia. 
Naye Padre Brian Lucas , Mkurugenzi wa Taifa wa Utume Katoliki Australia anasema karibu sehemu zote ambapo kuna Kanisa , wapo wanawake wenye ari, ambao wako mstari wa mbele na wengine hawaonekani , hawa siyo kwamba ni atawa tu bali wapo hata mamilioni ya wanawake walei wanao jitoa na wenye utajiri mkubwa wa imani.Anaongeza, “mfululizo wa picha na video  ni kuonesha dhamira kubwa kwa kutoa ufahamu kwa nini wanahamasisha wanawake hawa wa ajabu katika  upendo  huruma , na msamaha wao kwa sasa ili kutuhamasisha hata sisi” .

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.