2017-03-13 14:31:00

Mazungumzo ni njia mwalimu ya kuelekea amani na siyo kwa nguvu!


Mazungumzo ni njia mwalimu : amani inapatikana kwa njia ya mazungumzo, na siyo kwa nguvu : ni maneno kwa ufupi yaliyomo katika ujumbe wa Kardinali Philippe Ouédraogo Askofu Mkuu wa Ouagadougou nchini Burkina Faso alio utuma katika Jukwaa  la Kimataifa ambalo limefanyika kuanzia tarehe 3 hadi 7 Machi 2017 lenye  kuwa na  mada ya “mazungumzo ya kidini kwa ajili ya kuelemisha amani”.
Tukio hilo limeandaliwa kutokana na mwendelezo wa Jukwaa la kimataifa la tarehe 29 Mei 2015, likiwa na mada ya “elimu ya amani na maendeleo kwa njia ya mazungumzo ya kidini na utamadunisho”.  Jukwaa hilo lilifanyika huko  Cotonue nchini Bennin, kwa upendeleo wa  Albert Tévoedjeré,mjumbe maalum wa Umoja wa uchumi  na fedha Afrika Magharibi (UEMOA.) Wakati wa hotuba yake huko Ouagadougou Tévoedjeré , anathibitisha kuwa ili dini iweze kupinga chuki,kwanza  inahitaji kujifunza kusali kwa pamoja na kufanya kazi kwa pamoja ili kupunguza hali ya umasikini na hivyo, lazima Afrika iachane na maeno tu bali kuweka kwenye  vitendo  malengo ya dhati kwa ajili ya maendeleo ya Bara kwasababukwa kuishi  pamoja, uwezekano hupo wa maendeleo endelevu ya Afrika.


Naye Michaëlle Jean, Katibu Mkuu wa Mashirika ya  Kimataifa wa Afrika ya Magharibi(OIF),anasema ;utofauti wa tamaduni , na dini unajieleza kwa amani juu ya misingi ya umoja wa uzalendo na kijamii kwa urithi wa miongo hadi miongo. Kwa njia hiyo ni lazima kujenga msingi kwa vijana juu ya mazungumzo ambayo ndiyo nyenzo asili. Umuhimu wa mazungumzo umesisitizwa pia  Waziri wa Biashara ya nchi za nje  Aphan Barry ambaye amesema kwamba, ndilo jambo linakosekana  kwa sasa , kwasababu hiyo inajionesha kutokana na vurugu na  machafuko mengi ya kikabila na dini. Anaongeza,”Furaha ya kuishi pamoja ndiyo urithi wa Burkina faso.  Utamaduni na dini zetu  vina thamani ambavyo vinawawezesha kushinda mambo mengi na kuleta maelewano”.
Pamoja na wengine  waliyo toa hutuba katika Jukwa hilo , ni pamoja na mwakilishi wa UNESCO na Fiermini Eduardo Matoko Mkurugenzi Mkuu akikumbusha , lengo la  miaka 10 ya Kimataifa kwa ajili ya kukaribia utamaduni ;ni azimio lililotolewa na Umoja wa Mataifa kuanzia mwaka  2013-2033,lilo jikita  juu ya utofauti wa utamaduni, kabila, lugha na dini kwa kuhamasisha mazungumzo.Katika jukwaa hilo, pia kazi za makundi na kushirikishana wawakilishi wa taasisi, madhehebu mbalimbali walishiriki kikamilifu.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.