2017-03-10 17:00:00

Ni kwa njia ya Roho Mt. tunaweza kutambua Yesu ni Bwana!


Padre Raniero Cantalamessa  mhubiri wa nyumba ya Kipapa, tarehe 10 Machi 2017 ameanza kutoa tafakari za Kwaresima zinazoongozwa na kauli mbiu “Wala hawezi mtu kusema, “Yesu ni Bwana” Isipokuwa katika Roho Mtakatifu”. (1Kor. 12:3.).Akianza tafakari yake amesema, akisoma katika utangulizi wa sala ya Dominika ya kwanza ya Kwaresima ya mwaka huu, ni jambo moja limemwingia ndani. Katika sala hiyo haisemi , Mungu aweze kutujalia nguvu za kutimiza matendo ya huruma kama ulivyo utamaduni wa kipindi hiki, cha kufunga , sala na kutoa sadaka, bali sala inaomba kukua kwa utambuzi wa fumbo la Kristo.  Kwa njia hiyo anasema hakika hayo ni matendo ambayo Mkombozi anapendelea, na ndiyo lengo lake la kutoa mchango wa tafakari ya kwaresima kwa mwaka huu.

Padre anasema kwa kufuata takafari ya mwanzo katika kipindi cha majilio juu ya Roho mtakatifu ambaye anapaswa aongoze maisha na hata katika kutangaza Kanisa , katika tafakari ya kwaresima , ni kutafakari sehemu ya tatu ya  sala ya Nasadiki. Kwa maneno mengine katika tafakari hii ni kuona jinsi gani Roho Mtakatifu anatoa utangulizi wa kweli juu ya Kristo , na fumbo la Pasaka .Kwa kutafakari  kwa kina kuona jinsi Roho mtakatifu anakwenda sambamba na kifo na ufufuko wa Kristo nyuma yake, katika kifo chetu na hata katika ufufuko wetu. Katika sehemu ya pili ya Kanuni ya Imani inaelezea juu ya kuamini Bwana Yesu mzawa wa peke wa Mungu Baba , mwanga kwa mwanga  na Mungu kweli na kuishia kwa ajili yake vyote vimumbwa  naye…Pade Raniero anasema katika sehemu hiyo kuna hatua mbili tofauti za Imani , yaani nasadiki wa Bwana Mmoja Yesu kristo , inatafakari ukweli wa imani ya Kanisa mara baada ya pasaka.Inayo fuata mzawa wa kwanza wa Mungu , unaanza hatua ya kwanza ya utambuzi wa Kristo.

Mtakatifu Paulo anadhibitisha  kuwa Yesu Kristo anajionesha kama mwana wa Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu (Rm1,4) hadi kufika kwamba hakuna ambaye aweza kusema Yesu ni mwana wa Mungu kama siyo kwa njia ya Roho Mtakatifu” (1 kor 12, 3),hiyo ina  maana ya kuangaziwa kwa kina neema Na ni kwa njia ya uwezo wa nguvu ya  roho Mtakatifu tu, waamini wataweza kutambua kwa kina upendo wa Kristo unaozidi utambuzi” (Ef 3, 16-19).
Katika Injili ya Mtakatifu Yohane anasema matendo ya roho huyo mi msaidizi, ambaye anaweza kuwasaidia mitume watangaze yote aliyosema na kuwafikisha katika ukweli juu ya uhusiano uliopo kati yake na baba yake , na kwamba wao pia watakuwa mashahidi(Yh 16, 7-15).Roho mtakatifu daima anaongea akigusia Kristo, na roho Mtakatifu huyo hafanyi mambo mapya, bali anafanya mambo yaliyopo yawe mapya, yeye haongezi au kubadilisha , bali  yaliyopo anayageuza yawe mapya.Kwa ujio wa Roho mtakatifu wakati wa Pentekoste , kwa ghafla mambo mengi juu ya kristo yameonekana.

Padre Raniero akikumbusha mahubiri ya kwanza ya Petro, na kusema kwa sasa mahubiri ya kwanza ya Petro leo hii  tunaweza kutasifiri kama Baraka ya Baba Mtakatifu kwa ulimwengu mzima anayoifanya “urbi et orbi”:Tangu wakati wa mahubiri hayo , jumuiya ya kwanza walianza kusoma maisha ya Yesu mwenyewe ,juu ya kifo na ufufuko wake kwa namna nyingine, ambayo ni wazi utafikiri pazia iliyo anguka  toka machoni pao( 2 Cor 3.16).Pamoja na kuishi naye Yesu, bila kuangaziwa na roho mataktifu wasingeweza kutambua fumbo hilo.Katika kutambua fumbo la Yesu tutazame utambuzi wa  Yesu mwenyewe katika fumbo lake. Hii ina maana ya kwamba  inawezekana kabisa kutambua tu Yesu  anachofanya kwa ajili yangu , zaidi ya kile anachofanya kwa ajili yake.Mtakatifu Paulo anatusaidia kutambua vema ni kitu gani Yesu alifanya kwaajili yetu  na hasa kwa namna ya pekee katika matendo ya fumbo la Pasaka. Mwinjili Yohane anaeleza kwamba, Kristo ni neno la uzima aliyekuja kwetu sisi na ni kitu kimoja na Baba(Yh10,30)na zaidi anatuonesha kwamba Kristo anaonekana wazi,na kwa upande wa Mtakatifu Paul Kristo ni Mkombozi.

Padre Raniero anaeleza zaidi juu ya Historia ya Kanisa kwa upande wa kutambua vema  Yesu Kristo kwa miongo mingi , na kusema kuwa tunatambua matokeo pia ya utafiti wa Yesu kihistoria ya kwamba wengine walishindwa kumtumbua vyema, kama hata leo wengine wengi wanashindwa. Anatoa mfano kwamba historia ya Yesu ilikuwa kama ya watu wengine kama vile Mtakatifu Francisko wa Asisi , Yeye hakuishi moja kwa moja katika historia , bali yeye aliunda historia,hata leo katika historia ya uumbaji. Anatoa mifano ya waandishi wa historia nyingi , na kusema kuwa wapo wanahistoria wengine wanaotaka kuonesha namna ya kubagua historia ya uumbaji na kuweka ile ya ulimwengu kama vile ndiyo inaweza kueleweka zaidi , kwa kuitenganisha kama mawimbi na kuichukua ile ya asili.Lakini historia iliyo anzishwa na Yesu au mawimbi aliyo weka ni imani ya Kanisa , ikiongozwa na Roho Mtakatifu, na kwa njia hiyo inazidi kupanda hadi kufikia chemichemi yake

Mtakatifu Paulo anaongea juu ya tumbuzi wa Kristo kwa ngazi ya juu kabisa inayowakilisha,kumtambua na pia kumtangaza Bwana (Fil 3, 8). Ni tangazo linalounganisha imani na ufufuko wa Kristo , unao ufanya mtu aliyekombolewa:kama kinywa chako kitatangaza Yesu kuna Bwana na moyo ukaamini kwamba Mungu alimfufua  kutoka katika wafu, utaokoka! (Rom 10,9). Kwa sasa utambuzi huo umewezekana kwa njia ya roho mtakatifu(1Cor12, 3).Kwa maana hiyo kila mmoja ndiyo anaweza kutamka kwa mdomo wake maneno yale, bila kuwa na roho lakini maneno hayo hayawezi  kuwa na maana mara baada ya kutamkwa kama yale maneno ya yle aliyekombolewa kweli,Padre Cantalamessa anasema. Je kuna nini  cha muhimu katika udhibitisho wa Yesu ni Bwana? Ni kwasababu maneno hayo yana historia yake ya msingi wa fumbo la Pasaka.

Ni maneno yaliyotokana na matukio mawili ya kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu , na amefufuka kwa ajili ya haki yetu na hivyo ni Bwana. Na kwa njia hiyo ni kweli Yesu alikufa ,amerudia maisha ili awe Bwana wa walio kufa na hai(Rm 14,9).Matukio hayo ni mbegu iliyo katika habari njema ya kutangaza Kristo baadaye.Kwa njia ya kumshuhudia Yesu katika kutangaza ni jukumu letu sisi .Na kwamba anayetangaza maneno haya ina maana ya maisha; kwa kusema wewe ni Bwana wangu, niko chini yako ninakutambua kwa uhuru wote ya kwamba wewe ni mkombozi wangu, kiongozi wangu, mwalimu wangu na mwenye kuwa na uwezo na haki juu yangu.Mimi ni wako ni sehemu ya maisha yako moja kwa moja kwa sababu umeninunua kwa gharama kubwa (1 Kor 6, 19 ).

Padre Catalamesaa anasema hata kama kuna mihungu mingi ambayo yawezekana ikawapo duniani na mbingni, na kwa hakika mihungu na mabwana wapo , lakini kwetu sisi tunaye Mungu mmoja ambaye ni Baba na  ambaye kila kitu kinatoka kwake na sisi sote ni wake , na tunaye Bwana mmoja Yesu Kristo , ambaye kwake vitu  vyote vipo na vimeumbwa na sisi ndani yake tunaishi(1Kor 8,5-6). Hayo yaliandikwa na Mtakatifu Paulo wakati wa imani ya wakristo inaanza kukabiliana na baadhi ya tamaduni  na dini zilizokuwa zinazataka kutawala .Na hivyo uvumbuzi wa mwanga wa Yesu kama Bwana , ni habari mpya ya neema ya Mungu ambayo inatukumbusha hata sasa katika Kanisa. Maana ya Roho Mtakatifu kutufanya tuwe na utambuzi wa Kristo upo katika kumtangaza ya kwamba Yesu ni Bwana , mlango wa kutusaidia tuweze kutambua kikamilifu Kristo Mfufuka na anaishi! na siyo Yesu kama mtu mwingine yeyote yule , bali mtu wa aina yake , siyo wa kusoma katika vitabu na mafundisho yanayo sema uongo juu yake ,siyo kitu cha tamaduni au kumbukumbu, bali ni mwenye nafsi anayeishi na daima yupo katika roho.

Elimu hii ya kiroho  na maisha ya Yesu , kama Bwana haina maana ya kupuuza maarifa na lengo la mafundisho ya Kanisa la Kristo, bali ni kutaka kutoa uamsho wake. Anasema mmoja wa mababa wa Kanisa Mtakatifu Ireneus kuwa shukrani kwa Roho Mtakatifu ukweli umebainishwa kama amana yenye thamani zilitunzwa katika chombo chenye thamani,daima linapendeza na kufanya chombo kilichotunza kuwa muhimu. kwa nji hiyo moja ya mafundisho ya Kanisa , katika sehemu ya pili ya Nasadiki isemayo “aliye zaliwa bila kuumbwa , mwenye umungu pamoja na Baba “ndiyo itakuwa sehemu ya pili ya tafakari ijayo. Anasema Padre Cantalamessa.Anamaliza kwa kuwashauri wajisomee   Waraka wa Kitume wa Baba Mtakatifu Francisko juu ya Injili ya Furaha, akinukuu maneno yake yasemayo “Nanawakaribisha Wakristo wote, katika nafasi yoyote na hali, kugeuka  upya leo hii ili kukutana  na Yesu Kristo binafsi  au angalau kufanya uamuzi wa kumruhusu kukutana ,au kumtafuta yeye kila siku bila kuchoka kwani hakuna sababu kwa nini mtu anaweza kufikiri kwamba mwaliko huu siyo kwa ajili yake.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.