Baba Mtakatifu Francisko baada ya kumaliza mafungo ya Kiroho Ijumaa asubuhi ya
tarehe 10 Machi 2017 ametoa hotuba kidogo ya kutoa shukrani kwa Padre Julio Michelini
aliye waongoza kwa tafakari ya mafungo yao na kusema , anapenda kumshukuru kwa mema
aliyo watendea na zaidi namna alivyo jionesha kwao , kama asili kwa maana ya ukawaida
japokuwa yeyey ana uzoefu wa taalumua yake ya kimasomo , uandishi wa vitabu, marafiki
wazazi, vijana , ndugu zake wadogo wa jumuiya anao ishi nao .
Pili Baba Mtakatifu Francisko anamshukuru kwa kazi aliyo ifanya na jinsi alivyojiandaa.Hii
ina maana ya wajibu, yaani kuchulia mambo kwa uzito unaostahili.Anamshukuru kwa yote
aliyo wajalia na kusema, hakika ni kweli kuna mlima wa mambo ya kutafakari , lakini
pia anakumbusha kuwa Mtakatifu Ignatius anasema wakati wa mafungo ukijisikia faraja
au ukiwa ni lazima mambo hayo kuacha hapo,usisonge nayo mbele .Kwa hakika kila mtu
ameweza kupata moja au mawili kati ya hayo yote.
Licha ya hayo siyo kupoteza , inabaki, itatumika kwa wakati mwingine: na pengine
ni mambo mihimu na yenye nguvu, kwa wakati wengine haiwagusi chochote . labda ni neno
dogo tu linaloweza kujikita zaidi.Anatoa mfano baba Mtakatifu Francisko, kama muhubiri
mmoja wa Kihispania baada ya kutoa mahubiri yake makubwa na aliyo kuwa ameandaa vizuri
,Mtu mmoja alimwendea na mdhambi akiwa na machozi akamwomba aweza kuuungamishwa .
Alimuungamisha dhambi nyingi na machozi mengi. Muungamishi huyo alibaki kinywa wazi
kwasababu alikuwa anafahamu maisha ya mtu huyo.Wakati huo alimuulizia niambie ni wakati
gani umesikia kwamba Mungu amekugusa moyo wako?, na ni katika neno gani?. Aliposikia
maneno hayo, yeye alianza kucheka , na wakacheka wote, kwa namna hiyo wakati mwingine
maneno rahisi ni yale yanayotusaidia au yale magumu zaidi, kulingana na Bwana anavyotoa
neno mwafaka .
Shukrani nyingi na uendele kufanya kazi kwa ajili ya Kanisa ,ndani ya Kanisa na kutoa
mafundisho ya neno kwa mambo mengi ambayo Kanisa linakukabidhi. Lakini zaidi matashi
mema ya kuwa ndugu mwema.
Sr Angela Rwezala
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |