2017-03-08 15:50:00

Ziara ya Baba Mtakatifu Parokia ya Mt.Magdalena wa Kanosa 12.3.2017


Jumapili 12 Februari saa 10 za Jioni Baba Mtakatifu Francisko atatembelea Parokia ya Mtakatifu Magdalena wa Canosa .Atapokelewa na Askofu Msaidizi wake wa Jimbo la roma  Kardinali Agostino Vallini, Askofu msaidizi wa eneo la Magharibi ya Roma Paulo Sevadagi , Padre Giorgio Valente Mkuu wa Shirika la Wana wa Upendo (Kanosa),kwa upande wa wanaume ambaye alipewa majukumu ya  kuongoza Parokia hiyo tangu mwaka 1988. Vilevile paroko Padre Giorgio Spinello, msaidizi wake Padre Romeo Vettorato ,Padre Sergio Pinato , Padre Sandro Santoni na  wahudumu wa Parokia.
Wakati wa hija yake ya kitume kwenye Parokia hiyo, Baba Mtakatifu atakutana na vijana , watawa kike wa Shirika la mabinti wa upendo  na mkuu wao Annamaria Babbini, vilevile wagonjwa, wazazi wa watoto waliobatizwa mwaka 2016, wahudumu wa kichungaji wa parokia .Halikadhalika Baba Mtakatifu atatoa huduma ya Sakramenti ya kitubio kwa  watu wanne na baadaye kuadhimisha misa takatifu.

Parokia  ina idadi kubwa ya vijana na familia ambayo atakutana nayo Baba Mtakatifu Francisko Jumapili 12 Machi 2017.Ni Parokia ambayo Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili alitoa zawadi kwa wanashirika la Upendo  Canosiani wanawake na wanaume wakati wa tukio la Kutangazwa Mtakatifu mwanzilishi wao Mtakatifu Magdalena wa Kanosa , tukio lilitokeat arehe 2 Oktoba 1988.Misa ya kwanza iliadhimishwa tarehe 24 Machi 1996 na Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili akatembelea Parokia hiyo tarehe 21 Aprili 1996.

Sr. Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.