2017-03-08 16:05:00

Wanawake wanao uwezo mkubwa wa kuchanganya ukarimu na nguvu


Asubuhi ya terehe 7 Machi 2017 katika Ofisi za Shirika la Habari la Vatican kulikuwa na mkutano wa kikundi cha wanawake wa kudumu katika Baraza la Kipapa kwa ajili ya utamaduni.Kikundi hicho kimeundawa ndani ya Baraza hilo tangu Juni 2015 kwa ajili ya kutoa fursa  na kuendeleza sauti ya wanawake ndani ya Baraza la Kipapa.Ni kikundi cha wanawake 37 chini ya  mratibu Consuelo Corradi  Gombera wa Chuo Kikuu Lumsa Njini roma katika utafiti na mahusiano ya kimataifa.Mkutano huo umefanyika ukiwa na lengo la tukio la siku ya wanawake duniani, iliyofikia kilele chake tarehe 8 Februari 2017.
Katika kuwakilisha masuala ya wanawake, Kardinali Gianfranco Ravasi , Rais wa Baraza la Kipapa la Utamaduni,alikuwapo na kutoa hotuba yake.
Kufika kipindi kifupi kilicho malizika,nasema,hapakuwepo hata mwanamke mmoja katika Baraza la kipapa la Utamaduni, kwa maana hiyo bado ilikosekana ukamilisho wa  mfano wa sura ya Mungu.Ni maneno ya nguvu ya Kardinali Ravasi kwenye ufunguzi katika hotuba yake juu ya masuala ya wanawake.Yeye kama mtaalamu wa Biblia anawakumbusha kuwa, Mungu aliumba binadamu kwa mfano wake mme na mke aliwaumba.Kwa namna hiyo katika kukamilisha Baraza la Kipapa la Utamaduni uwepo wa wanawake umebadilisha mambo.Na kwamba kuanzisha mpango huo ni mchango mkubwa wa Kanisa kujitoa kwa ajili ya wanawake

Aidha anasema Kardinali Ravasi , ya kwamba mpango wa wanawake utaka zaidi kutoa mtazamo wa wanawake katika shughuli za Baraza la kipapa . Mchango wao unaweza kutolewa kwa ngazi mbili. Sehemu ya kwanza ni ile ambayo hadi sasa Baraza lilikuwa halijafikiria na kwamba ni sehemu mojawapo ya uzoefu wa wanawake, na kwa uzoefu wa kazi ya wanawake hata walei .Jambo la pili ni ule mtindo wa kuweza kwa pamoja kusoma mengi zaidi kwa mtazamo wa ujulma hali halisi , mada zinazokabili baraza,hasa kwa kuachilia mbali na kasumba za uchambuzi wa kiteolojia na kifalsafa ambayo ndiyo hakika lugha ya Kanisa.Hata hivyo Baba Mtakatifu Francisko hivi karibuni katika mojawapo ya mahubiri yake kwenye Kikanisa Kidogo cha Mtakatifu Marta mjini Vatican  alisema juu ya suala la mwanamke kuwa  siyo sababu za kutazama masuala ya kazi na  nafasi ya mwanamke katika Kanisa ,bali inapaswa kuwa  mchango wa kifikra, hata tafakari.Kwa njia hiyo hata  Kardinali Ravasi anasema siyo kwamba anasema wanawake wanaingia ndani ya Baraza lao kwaajili ya kujaza nafasi wazi au kwa mantiki ya ukamilisho wa uumbaji tu, bali wanawake wanaingia ndani ya mfumo wa Baraza katika sera ya utamaduni.

Mkutano huo umeweza kuwakilisha wakufunzi wa Chuo Kikuu, wajasiriamali, wadau wa kisiasa, wasanii, waandishi wa habari.Watawa wawili, wawakilishi wawili wa kazi kutoka Vatican, akiwemo mwandishi wa habari wa Radio vatican Roberta Gissotti na Micol Forti, Muhusika wa ukusanyaji wa sanaa za kisasa katika Jumba la Makubusho Vatican.Watu wengine ni  kutoka katika utamaduni na kijiografia , hata kimadhehebu kama Mtaalamu wa mambo ya kiislam kutoka Iran Shahrazad Houshmand.Mratibu wa mkutano huo kuhusu masuala  na tafakari katika kutazama kwa ndani mandhari na tofauti za wanawake  Daktari Corradi anasema Wanawake ni tofauti na wanaume.Usawa wa haki hauna maana ya kupoteza utofauti .Je ni utofauti gani iliyopo kati ya mwanaume na mwanamke? Anatoa jibu ya kwamba ni uwezo wa kujua kuchanganya ukarimu na nguvu. Hivyo wanawake nikutaka  kuwa mashuhuda wa wanaume na kuwaonesha  kwamba wana uwezo wa  kuwa na huruma  wakati huo huo, kuteseka na kufurahi na wangine bila kupoteza nguvu yao binafsi.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.