2017-03-07 12:09:00

Mafuriko yasababisha majanga makubwa nchini Zimbabwe


Zaidi ya watu 250 wamekwishafariki dunia kutokana na mafuriko ambayo yameikumba Zimbabwe tangu mwezi Desemba, 2016. Zimbabwe ni kati ya nchi za Kiafrika ambazo zimeathirika vibaya sana kutokana na ukame wa muda mrefu na kwamba, kwa sasa kuna Zaidi ya watu elfu mbili hawana makazi maalum baada ya nyumba zao kuchukuliwa na mkondo wa maji. Kwa sasa watu wengi wanahitaji mahema, dawa pamoja na chakula cha dharura. Hayo yamsemwa na Bishow Parajul, Mratibu wa Programme ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa nchini Zimbabwe.

Taarifa zinaonesha kwamba, eneo lililoathirika vibaya kwa mafuriko ni Wilaya ya Tsholtsho, iliyoko Kusini Magharibi mwa Zimbabwe. Eneo hili kwa muda mrefu liliathirika kutokana na ukame, maarufu kama ”La Nina” lakini sasa kuna mvua kubwa za”El Nino” ambazo zinaendelea kusababisha madhara makubwa kwa watu na mali zao. Serikali ya Zimbabwe imetangaza eneo hili kuwa ni sehemu janga la kitaifa, kumbe linahitaji msaada wa dharura ili kuwasaidia watu walioathirika kutoka na mafuriko yanayoendelea huko Zimbabwe!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.