2017-03-07 16:00:00

Kwa kufanya maamuzi Yesu anaomba kwa njia ya kipawa cha Roho


Mwaliko wa kujiuliza iwapo kweli nasikiliza sauti ya Petro na walio wadhaifu , namna gani tunafanya maamuzi, kama katika maisha kuna mikakati ya kutokumfuata Yesu hadi mwisho ni kati ya mafundisho ya Padre Giulio Michelini ametoa wakati tafakari ya sehemu ya kwanza ya  mafungo ya kiroho kwa Baba Mtakatifu Francisko na Sekretarieti yake, mada ya mafungo kuhusu mateso , kifo na ufufuko wa Yesu kutoka katika Injili ya Mtakatifu Matayo. Ni mada aliyopendelea kuwaongoza kwa kipindi hiki cha mafungo. Ni washiriki 74 katika mafungo ya kiroho kwenye nyumba ya mafungo ya Kiroho  iliyopo Aricia kando ya Mji wa Roma, mafungo ya kifroho yanayotazamiwa kumalizika Ijumaa tarehe 10 Februari 2017.

Petro kumkiri Yesu wakati wa safari yao kuelekea Yerusalem ndiyo umekuwa utangulizi wa tafakari ya kwanza asubuhi ya tarehe 6 Februari 2017.Bwana aliweza kukamilisha safari yake kuelekea katika mji Mtakatifu,kama ielezavyo Injili ya Mtakatifu Yohane katika sherehe tatu za hija ya wayahudi.
Padre Michelini anasema Yesu anachotamka ni tofauti na wengine , kwani mara ya mwisho anatamka juu ya  mateso, kifo na ufufuko wake, ambayo tunaweza kuita aina tatu zinazofanana katika Injili tatu,na katika mwinjili mwanzo anaonesha matukio haya: Yohane mbatizaji, Ubatizo wa Yesu na majaribu. Ni muhimu kutazama mfululizo wa matukio hayo kama vile Petro anamtambuaYesu kuwa ni masiha, Yesu anatamka juu ya mateso yake , na pia Yesu anajibadiloka  juu ya mlima.

 Kwanini katika Injili ya Mtakatifu Matayo tangu mwanzo anaelezea safari yake ya mwisho kulekea Yerusalem?.Padre Michelini anauliza akikumbusha kwamba Yesu pamoja na kuongea kama maneno ya Baba , pia anamsikiliza Petro ,anakubali  kuvikwa cheo cha masiha , pamoja na kwamba hiyo itajidhibitisha wazi kwa namna ya unyenyekevu na mwanamke huko Betania.
Vinginevyo kulingana na historia  za watu kale, Padre Michelini anatoa mfano wa mtawala Alexandre Magno kwani anasema; kwa mujibu wa wasifu wake, alipokuwa akitaka kufanya maamuzi alitumia mantiki ya kichawi, na kwenda kutafuta ushsuri wa waganga wa kienyeji.Lakini Yesu hakufikia katika imani hii ya  kutumia waganga wa lienyeji na wala kutafuta ushauri wao, au kwa njia ya ndoto. Hakuna katika Injili yoyote inayoelezea au kuonesha kuwa Yesu aliota ndoto.Yesu anafanya tendo la maombi, kwa njia ya kipawa cha Roho Mtakatifu, na kwasababu hiyo baba yake anaongea naye kwa sauti ya unyenyekevu.

Katika mapokeo ya Wayahudi , anaendelea Padre Michelini waliamini kuwa Mungu angejibainisha kwa njia ya watoto , ndoto , mambo , sauti ndogo : hizo zote zilikuwa ni njia za kusema kwamba mawasiliano yanawafikia kwa njia ya kawaida na wala siyo kwa  nguvu au iliyolazimishwa bali inayo fanana na upepo mwanana ulio mpulizia hata Eliha katika mlima wa Horebu .Yesu ni myenyekevu wa moyo, anasikiliza sauti ya Petro na tangu wakati huo anakubali matokeo yake, na matendo yake,hakuweza tena kujiondoa tena, bali alitangaza kifo na ufufuko wake huko Yerusalem 
Na mwisho wa Tafakari hiyo Padre Michelini anawashauri wajiulize kwa kina kwa njia ya maswali ya moja kwa moja kama vile uamuzi wangu una maana gani , siyo kwenye mambo madogo ya uamuzi wa kila siku , bali uamuzi muhimu wa kuchukua katika maisha .Kwa mantiki gani nifanya uchaguzi? Naamua kwa kukurupuka au nafanya kama kawaida , je najiweka binfsi mbele ya ufalme wa mungu na wengine , nasikiliza sauti ya Mungu  lakini ambaye anaongea kwa unyeyenyekevu?

Sehemu ya pili ya maswali juu ya tafakari ni kuhusu sauti inayo ongea kama watoto, au mambo ambayo ni dhaifu kama ndoto au sauti ya kina.Anasema Padre Michelini kuwa,siyo kwa bahati mbaya kwasababu hata Baba aliongea kwa njia ya  Simoni Petro alivyo mkiri Yesu: Yesu katika ubinadamu wake, ni kama vile Mtakatifu Francisko wa Asisi, walitambua ya kwamba Mungu anajionesha kwa njia ya mitume na hata mitumewadogo.Kwa njia hiyo Padre Michelini anawauliza maswali je  ninao utii wa kusikiliza Petro ?, upo unyenyevu  wa kusikiliza wengine walio wadhaifu au ni kusikiliza sauti zetu zinazoongea kwa wengine?.Swali la tatu la kujitafakari, Padre Michelini , amewaalika kutazama mikakati ya maisha, na kujiuliza  kama nakubali au hapana kwenda hadi mwisho katika kumfuasa Yesu Kristo , pamoja na kuwa  inahitaji kuchukua msalaba kama alivyo mweleza mara moja mtume Simon Petro baada ya kumkiri kwake; “anayetaka kunifuata , ajikane mwenyewe na kuchuka msalaba kunifuata”.

Sr Amgela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.