2017-03-06 15:33:00

Soma ujumbe wa Biblia kama usomavyo ujumbe wa simu ya mkononi


Waamini wanapaswa kujenga utamaduni na mazoea ya kusoma, kulitafakari na kulimwilisha Neno la Mungu katika maisha yao mara nyingi kama wafanyavyo kwenye simu ya mkononi, kufanya hivyo ni kupambana dhidi ya mabaya na kuwa karibu na Mungu na kuelekea njia ya wema.Huo ndiyo ushauri mkubwa wa Baba Mtakatifu Francisko maeutoa wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili tarehe 5 Machi 2017 wakati Kanisa linaadimisha Dominika ya kwanza ya Kwaresima, kwenye uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Katika Dominika ya kwanza ya Kwaresima , Injili inatoa utangulizi wa safari kuelekea Pasaka , ikionesha Yesu anabaki  kwa kipindi cha siku arobaini Jangwani , lakini anajaribiwa na shetani (Mt 4,1-11.)Matukio hayo yanajitokeza katika kipindi cha maisha ya Yesu mara baada ya ubatizo katika mto wa Yordani na kuanza utume wake kwa watu wote.Wakati huo huo  yeye alikuwa amemaliza kuwekewa wakfu wa roho Mtakatifu na kusikia sauti kutoka mbinguni ikisema huyu ndiye Mwanangu mpendwa (Mt 3,17).

Yesu yuko tayari kuanza utume wake pamoja na kwamba anaye adui ambaye tayari kajitangaza shetani , anamkabili mara moja , uso kwa uso.Shetani anaanza na maneno ya majaribu ya kutamka Mwana wa Mungu ili kumfanya asiweze kukamilisha utume wake, akisema kama wewe ni mwana wa Mungu kwasababu “Hiyo ni kwasababu shetani anataka atimize miujiza kama wafanyavyo viinimacho, kwa mfano wa kubadili mawe yawe chakula cha kushibisha njaa, au kujitupa toka kileleni maana anadai atapokelewa na malaika.Baada ya majaribu mawili anaongeza la tatu , kuabudu shetani ili aweze kupata madaraka ya ulimwengu.

Katika majaribu hayo matatu, shetani anataka amwondelee Yesu njia ya utii na unyenyekevu kwasabu anatambua vema ya kwamba kumwondelea hayo mabaya , ubaya utakuwa umeshinda , kwa kupata njia fupi na za uongo katika  kupenda makuu na utukufu.Baba Mtakatifu anasema lakini sumu zote kutoka kinywani mwa shetani, zinazuiwa na mshale wa maneno ya Mungu (4,7.10) yanayoeleza matashi ya Baba.Yesu hakujibu zaidi ya kutamka maneno ya Mungu na kwa kujazwa na roho Mtakatifu anatoka na ushindi Jangwani.

Katika kipindi chote cha kwaresima, kama wakristo tunaalikwa kufuata njia ya Yesu, kukabiliana na mapambano ya kiroho dhidi ya nguvu ya ibilisi kwa nguvu ya neno la Mungu.Maneno yetu tu hayatoshi , bali ni kwa njia ya maneno ya Mungu yanashinda nguvu za shetani.Kwa namna hiyo inabidi kuwa na mazoe ya Biblia, kuisoma mara kwa mara na kutafakari kwa kina.Kwani Biblia ni neno la Mungi ambalo linafanya kazi daima na makini.
Baba Mtakatifu Francisko amewauliza , ni jambo gani linaweza kutokea iwapo tunatumia Biblia kama tunavyotumia simu zetu za mkono?kama Biblia tuingeibeba katika mifuko yetu,au, kama tungerudi nyuma kuichukua mara baada ya kuisahau nyuma, kama tufanyavyo tunaposahau simu nyumbani? Kama tungefunua Biblia mara nyingi kwa siku tukasoma ujumbe wake kama  tusomavyo ujumbe wa simu ya mkono kwa siku? Ni kitu gani chaweza kutokea, anasisitiza Baba Mtakatifu!

Jibu analitoa Baba Mtaktifu akisema ;Kwa hakika kama tungeweza kuwa na Neno la Mungu daima katika mioyo yetu , hakuna kishawishi kingetufanya kuwenda mbali na Mungu na hata kizingiti chochote cha kuweza kupotea njia ya wema.Tungetambua  kushinda vishawishi vya ubaya kila siku vilivyomo ndani na nje yetu , tungejikuta tunaishi maisha yatokanayo na roho Mtakatifu na kuwapokea , kuwapenda ndugu zetu, na zaidi wale wadhaifu , wenye shida na hata maadui zetu.
Anamalizia kwa matashi mema  ya kumfuata mama Maria mfano wa  ya utii kwa Mungu, na matumaini ya utashi wake ambaye aweze kutusikindikiza katika safari ya kwaresima ili tupate kusikiliza kwa makini Neno la Mungu katika kukamilisha ukweli wa uongofu wa moyo.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.