Jumapili 5 Februari 2017 kwenye nyumba ya mafungo ya kiroho iliyoko mji wa Ariccia Roma , Baba Mtakatifu Francisko amaeanza mafungo akiwa pamoja na Sekretarieti Kuu ya vatican .Katika mafungo hayo kutakuwa na mada tisa za tafakari ya kwaresima , inayo ongozwa na Padre Giulio Michelini wa Shirika la ndugu wadogo wa Mtakatifu Francisko ambapo anawaongoza katika kutafakari mateso , kifo na ufufuko wa Yesu Kristo kutoka katika Injili ya Mathayo . Baada ya utangulizi wa mafungo Jumapili jioni, sikiu yaJumatatu wameanza na tafakari ya Petro kumkiri Yesu wakati wako njiani kuelekea Mji wa Yerusalem.Hata hivyo Baba Mtakatifu Francisko aliomba asindikizwe kwa sala na kwa ajili ya wenzake , kwa kipindi chote cha mafungo ambayo yatamalizika tarehe 10 Februari 2017 wakati wa kumaliza sala ya malaika wa Bwana na salam zake Jumapili 5 Febuari 2017.Taarifa inasema kuwa kwa kipindi chote cha mafungo, mikutano mbalimbali na hata katekesi ya jumatano ya Baba Mtakatifu vitakuwa vimesitishwa.
Kwa mtazamo wa mateso kama ilivyondikwa na Mtakatifu Mathayo , itakuwa na kama
vile kukaa mbele ya picha kubwa , kuitazama kwa pamoja ambapo labda inaweza kujikita
ndani ya moyo kwa kitu fulani.Hayo ni maelezo ya Padre Padre Michelini kwa utangulizi
wa mafungo anaelezea juu ya kitabu fulani toleo mwaka 2010 kinachoelezea juu ya vifo
vya kijujuu kwa watu wa kihistoria.Lakini anasema katika Injili zote zinaelezea kwamba
Yesu alikufa kweli na maisha yake siyo film .Maisha na kifo cha Yesu kwa hakika ni
vitu viwili sambamba. Kwa namna hiyo kila tafakari kwa siku hizo itaanza na sehemu
ya Injili ya Matayo juu ya mateso , kifo na ufufuko , kwa mtazamo wa kina wa maisha
yake ya kitume aliyo fanya huko Galilaya.
Aidha anasema , katika mafungo ya kiroho katika siku hizi pia ni namna ya kukaa na
Mtakatifu Petro.Kwa njia hiyo inabidi kufuata maelekezo ya “Injili ya furaha” , mahali
ambapo Baba Mtakatifu Francisko anawaalika wakristo kukutana na Yesu mwenyewe .
Kwa siki hizi Padre Michellini anatoa ushauri kwamba hata sisi sote tunaweza kufikiria kwamba wote tuko ndani ya kikundi cha wale wanao paswa kuinjilishwa .Siyo kwamba tuko katika tabaka la wasio mtambua Yesu ,na wala waliomo ndani ya wale walio batizwa ambao lakini wanaishi na mahitaji ya ubatizo, bali ni wale ambao uinjilishaji mpya umefikiriwa hawali ya yote kuwasha moto katika mioyo ya waamini ambao daima wako ndani ya jumuiya na wanafuata jumuiya .Padre Michellini anasisitiza zaidi akisema ni nyinyi ndugu mlio kiini cha unjilishaji , kwa papa , Sektratarieti ya Vatican katika kiindi hiki mwafaka ,na wote mnaalikwa kukaa pembeni na kusali.
Tafakari ya Padre Michelini ilianza na kwa kumtazama Mtakatifu Francisko wa Assisi alipo toa mahubiri kwa Papa Onorio wa II na makardinali Mwandishi Tommaso wa Celano anasimulia ya kwamba askofu wa Ostia alikuwa na hofu ya kwamba Mtakafifu Francisko wa Asisi angeweza kudharauliwa kwa maneno yake rahisi wakati wa kutoa mahibiri kwa Papa na Makardinali na kwa njia hiyo Padrea anasema naye kidogo ana hofu lakini ataweza kufanya awezacho , maana mahali amabapo hawezi fika Roho Mtakatifu atafanya hivyo.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.
All the contents on this site are copyrighted ©. |