2017-03-04 16:00:00

Wakristo Kaskazini ya Misri kuacha Sinai kwasababu ya vurugu


Wakristo  wengi wameyakimbia makazi yao huko Al Arich , makao makuu ya Serikali ya Misri ya Kaskazini, kwasababu ya vurugu mpya za kampeni  ya majeshi ya kijihadi (Daesh) dhidi ya wakristo wa kikopti walioko nchini Misri ya Mashariki.Habari kutoka Gazeti la AsiaNews , linasema ni zaidi ya watu 1500 wakoptiki wanao kimbia.Na kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Misri navyo vinaeleza kwamba ni kama familia 112 wamekimbilia katika mji wa Ismailya 120km Mashariki ya mji wa Cairo, mahali ambapo baadhi ya makanisa  ya kikopti  na wakristo wameweza kuwakaribisha, na wengine kupokelewa katika miji ya Qaliubiya, Assiout na katika mji mkuu wa Misri.Ukubwa wa eneo la Sinai Kaskazni wenye 61km za mraba ambao ndiyo kitovu kikubwa cha makundi ya kijihadi wanao pambana na nguvu za jeshi na raia. Tangu mwaka 2014 majeshi hayo yalijitangaza serikali ya Kislam kwenye Wilaya ya Sinai.Hali imezidi kuwa mbaya kwa wiki hizi mara baada ya kutokea mauaji mengi dhidi ya Jumuiya za kokpti na wakristo saba na wengine kuchomwa moto wakiwa wazima.

Meneno ya kulaani matendo ya kinyama namna hiyo yalitolewa pia na Imam Mkuu wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar , Ahammad al-Tayyib , wakati wa mkutano kuhusu  Uhuru na uzalendo kati ya utofauti na ushirikiano,  “ ulio andaliwa hivi karibuni mjini Cairo na Taasisi muhimu za kiislam chini ya matashi mema ya Rais wa Jamhuri ya Misri .Mkutano huo uliudhuliwa na viongozi  wawakilishi wa madhehebu mbalimbali na walei kutoka nchi 50.
Katika mkutano huo ,uli hutubiwa pia  na viongozi wa kiroho wa madhedehebu ya Kikristo kutoka nchi za mashariki  ulimalizika kwa kutoa azimio la mshikamano  kati ya wakristo na waislam ambao unalaani vikali vurugu kwa kutumia jina la dini na kuwataka watu wa imani tofauti kuishi kwa furaha katika umoja na kuheshimiana.

Miongoni mwa masuala yaliyo zungumzwa katika mkutano huo ni dhana  ya madai ya kuzingatia misingi ya dini ambayo inadaiwa kukosekana usawa wa kiraia kati ya Waislam na wasio kuwa waislam .Dhana hiyo hata Imam wa Tayyib alikubali kutokuwa na uwelewa zaidi .Hivyo juhudi inahitaji ya kuweza kujua vema na kuhamasisha juu ya umuhimu wa dhana ya uzalendo ambao ni msingi na  kwamba utashi wa pamoja katika kujenga taifa ni msingi mkubwa wa uzalendo , usawa sheria , vinginevyo ni kushindwa kwa maendeleo ya binadamu wote.
Mara baada ya mkutano huo viongozi wa Kipatriaki wa Maronite Bechara Boutros Rai na Patriaki Mkaldayo Louis Raphaele I Sako , wote wawili walikuwa maeudhuria mkutano juu ya "uhuru na uzalendo , tofuti na ushirikiano," walikutana na Rais wa Misri tarehe 2 Machi 2017 Mjini Cairo. 


Rais wa Misri Abdel Fattah  al Sisi amewambia viongozi hao kwamba “viongozi wa dini katika awamu ya sasa ya kihistoria , wana wajibu mkubwa katika kueneza kwenye nchi zote za Kiarabu msingi wa uraia , na kukataa tafsiri ya vitabu vitakatifu vya uongo na mafundisho ya dini zinazotumiwa na mashirika ya msimamo mkali na magaidi kama chombo cha kiitikadi kwa ajili ya mipango yao ya madaraka.Ikumbukwe hivi karibuni Rais wa Misri Abdel Fattah  al Sisi alikuwa tayari amesha sema juu ya haja kurudia upya mazungumzo ya dini katika nchi za Mashariki ikiwa ni mkakati dhidi ya migogoro ya madhehebu ya kidini ambayo yamekumba sehemu kubwa ya nchi  za Mashariki ya kati.

Wakati wa mazungumzo na maptriaki wawili katoliki kutoka nchi za Mashariki, Rais Al Sisi , akiongelea juu hali ya Misri kwamba siyo kubainisha waislam na wakristo kama wanachama wengi au wachache wa dini , bali anasisitiza haja ya  wote kujisikia washiriki wa nchi ya moja ya Misri na kutoa huduma bila ubaguzi wa dini,katika kuheshimu usawa kamili ambao umejengwa kwenye misingi ya uzalendo. 

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.