2017-03-04 14:46:00

Papa Francisko apokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi wa Iraq


Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 4 Machi 2017 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mheshimiwa Omer Ahmed Karim Berzinji, Balozi wa Irak mjini Vatican. Balozi Berzinji alizaliwa kunako mwaka 1960 ameoa na amebahatika kupata watoto wanne. Ana shahada ya uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Baghdad. Katika maisha yake tangu mwaka 1984 hadi mwaka 2004 alikuwa ni mwanachama wa Chama cha Mawakili nchini Iran.

Amewahi kufanya kazi katika Taasisi ya Sayansi za binadamu, Jumuiya ya Ulaya; Haki za binadamu katika Wizara ya mambo ya nje ya nchi na ushirikiano wa kimataifa. Kunako mwaka 2004 hadi mwaka 2009 Balozi aliyekuwa anashughulikia haki msingi za binadamu kwenye Wizara mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa. Kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2013 alikuwa ni Balozi wa Iraq nchini Lebanon. Mwaka 2013 hadi mwaka 2015 Balozi wa Iraq nchini Romania. Tangu mwaka 2015 amekuwa ni Katibu mkuu msaidizi wa Masuala ya Kisheria na Uhusiano wa Kimataifa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.