2017-03-04 10:22:00

Ni vipi kutambua wito wa Kristo kutoka sauti za mitandao ya kijamii?


Jinsi gani ya kutambua wito wa Kristo kwenye zama za mitandao ya kijamii? Jinsi gani ya kuwaongoza kwenye utambuzi wa miito , na namna ya kutofautisha , sauti za“uvumi mwanana wa upepo miongoni mwa sauti nyingi  zitolewazo na makampuni ya vyombo vya habari . Hayo ndiyo masuala ya mkutano juu ya vijana  utakao fanyika Barcelona kuanzia tarehe 28-31 Machi 2017  kwa  mada “ kutembea pamoja nao” kutoka katika Injili ya Mtakatifu Lk 24, 15.
Mkutano kuhusu namna ya kuwasindikiza vijana ili  waweze kujibu wito wao kwa kristo katika uhuru  umeandaliwa na Baraza la Maaskofu wa Ulaya , kwa ushirikiano wa Baraza la maaskofu wa Huspania na Jimbo Kuu la Barcelona.

Washiriki 200 na kati yako wapo maaskofu , wahusika wa masuala ya kichungaji kwa vijana shuleni , vyuo vikuu, miito katekesi ,hata mashirika mengine ya utume wa Kanisa kama vile chama cha Emaus, ambapo wataongozwa na tafakari ya Injili .Pia miongoni mwa wengi ni Makardinali Angelo Bagnasco na Vincent Nicholas Rais wa Baraza la Maaskofu Ulaya na makamu  wake, Pia Askofu Mkuu wa Jimbo la Barcelona  Juan José Omella Omella.
Taarifa zinasema kuwa mada inayohusiana na vijana na changamoto ya kuwasindikiza kwenye mantiki ya sasa ya kijamii ndiyo zitakuwa mada motomoto kwa siku nne  katika kubadilishana mawazo na hasa njia bora na uzoefu miongoni mwa washiriki.Pamoja na hayo, maadhimisho ya ibada za misa , sala na kuabudu vitawaongoza kwa siku hizo nne . Ili kutoa maana zaidi kwa mfano muhimu wa mapendekezo ya kutangaza Injili washiriki hao pia watafanya ziara katika familia takatifu.

Mtazamo wa Mkutano huo ni wazi unaakisi tayari maandalizi ya Sinodi ijayo kuhusu Vijana iliyotangazwana na Baba Mtakatifu Francisko kufanyika Vatican Oktoba 2018  ikiwa ni mada juu ya vijana na wito.Matunda ya kazi ya mkutano wa Barcellona yatapelekwa moja kwa moja kwa Mababa wa Sinodi.Halikadhalika inaleta maana kubwa suala la ushiriki wa Kardinali Lorenzo Baldisseri, Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu , ambaye atapata fursa ya kutoa machache ya kusema wakati wa kubadilishana mawazo na wahudumu wa kichungaji kwa vijana wakati wa Mkutano huo.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.