2017-03-03 14:24:00

Maombi ya kiekuemene yajenge vifungo vya undugu na kusaidiana


Siku ya kimataifa ya sala ya kiekumene inayo adhimishwa kila tarehe 3 ya mwezi wa tatu inatoa njia za tafakari na kushauri kwa mada ya kujiulize Nina haki na nyinyi?  (Mt 20,13) kwa kujenga upeo wa amani ulio jengwa juu ya haki , mazungumzo , mshikamano kwa kupinga daima chuki na vurugu , na daima kuthibitisha hadhi ya utu wa kila binadamu. 
Siku hiyo inawakilisha miongo kongwe ya kiekumene , iliyo anzishwa huko Marekani na vyama vya wanawake wa makanisa ya kikristo mwishoni mwa miaka ya 1,800 na baadaye ikazidi kupamba moto, hatua kwa hatua hadi kuwashirikisha hata waamini Katoliki na wa Orthodox , na hivyo kufikia leo hii ni zaidi ya nchi 170 katika mabara matano ya Dunia. Tangu mwanzo lengo lake ni kujenga vifungo vya udugu kati ya wanawake  kutoka katika asili mbalimbali katika kujikita kwenye  umoja ili mwishowe waweze kuwatumikia wasio jiweza  kwa kuwajibika zaidi katika kutafakari kwa upendo mkuu wa sura ya Mungu  wakiongozwa na kauli mbiu “kujifunza kuomba , na kuomba kwa ajili ya kutenda".

Mwaka hadi mwaka hali hiyo imeweza kutawanyika na kukumbatia maombi lakini pia maombi yanafuatana na ishara halisi ya mshikamano na nchi ambayo Kamati ya wanawake wa madhehebu mbalimbali kimataifa  wameandaa siku ifanyike. Hii ni njia kuu mzuri ya kujenga madaraja ya uelewano na upendo kati ya wanawake wanaoishi katika maeneo kijiografia ya mbali.Kufuatia tukio la Maombi ya ya kimatifa ya kiekumene kwa mwaka huu,Nakala ya ujumbe wa  2017 umeandaliwa na wanawake wa Ufillippini , ambapo ndani ya makala hiyo wameweka matumaini yao , uzoefu wao ,imani yao, na mateso yao.Na zaidi wametaka kutoa sauti kwa wale ambao kwa bahati mbaya hawana sauti , wanachotambua ni upweke , udhalilishwaji na uchungu.

Kwa mfano Katika makala yao zipo historia nyingi lakini miongoni mwa historia hizo ni ya kijana mwanamke mmoja Merliyn.Anasimulia juu ya mama yake ambaye kwa muda mrefu aliathirika  kwa unyanyaswaji ndani ya familia yake. Na akiwa na umri wa miaka saba, mama yake Merlyn alikufa kwa salatani . Na kwa bahati baada ya mwezi mmoja akashuhudia tena  kwa macho yake kifo cha baba yake aliyeuwawa kwasababu ya mabishano ya ardhi.Baada ya mwaka mmoja alilazimika kitafuta kazi kwa ajili ya kuwasaidia wadogo zake kwenda shule..
Kwa njia hiyo akiwa na mia 15 Mrlyn alipanda meli kuelekea mji mkuu , akiwa na matumaini moyoni mwake ya kupata kazi,  lakini kazi aliyoipata ilikuwa ni kutumika ndani ya familia moja.Baada ya kufanya kazi kwa miezi mitatu bila ya kupokea hata senti moja aliamua kuacha kazi hiyo , lakini mwenye nyumba akamsingizia wizi na hivyo akakamatwa na kuwekwa kuzuizini kwa siku tatu,katika jela ya manisapaa ya mji.

Kwa bahati nzuri ya mwanasheria mkristo aliyekuwa anatoa huduma ya bure  aliweza kumsaidia na kushinda kesi dhidi ya mwajiri huyo.Historia ya Merlyn ni kama nembo ya ugumu unao wakabili wafanyakazi wa ndani ya nyumba, na historia hiyo ndiyo hali halisi inayo wakumba wasichana wengi zaidi ya milioni mbili nchini ufilippini wanaolazimika kuondaka mashambani kuhamia maeneo ya mijini au nchi za nje.
Kutoka moyo wa wanawake Kifilipino wanatoa sala hii: "Ee Mungu, hatuwezi tena kupata udhuru; ni wakati wa kukabiliana uso kwa uso makosa yetu. ni wajibu wa kutokuweza kijibidisha japokuwa umesikia kilio cha watu wako. Ni wakati wa kujibu wale wanahitaji haki,utusamehe ee Mungu na utupatie uhuru ili tuhamasishe kwa matendo.
Wanawake hao wameweza kwenda mashamba ya mpunga kawasaidia watu jirani wakati wa kupanda na wakati wa  mavuno .Hakuna mtu anaye lipwa bali mavuno ni kwaajili ya kugawana kwa wote ,hii desturi yao inaitwa Dagyaw.Dagyaw ni desturi nzuri ya kujenga na kufanikisha jamii. 

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.