2017-03-03 15:18:00

Kukosa chakula ni pamoja na ukosefu wa usalama na usimamizi


Kanisa haina sababu ya kupinga serikali, bali lengo lao ni kuhakikisha kwamba wanajitahidi katika kutoa msaada kwa ajili ya mipango ya amani.Ni taarifa iliyotolewa na Askofu Erkolani Lodu Tombe wa Jimbo la Yei kwenye Shirika la Habari akitazama  matukio ya hali ya kutisha nchini Sudan Kusini , mahali ambapo kwa miezi mitatu zaidi ya watu 100,000 wamekimbia makazi yao. Habari zinasema, mkusanyiko wa watu wamefika katika makambi nchini Uganda, wanaeleza mateso na ukukwaji unaofanywa na wanajeshi,hata hivyo Umoja wa mataifa hivi karibuni walikuwa wameripoti juu ya ubakaji, mauji ya raia na hofu ya kukamatwa, kwamba ndiyo miongoni mwa sababu kuu zinasosababisha maelfu ya watu kukimbia nchi yao. Hii ni dharua kubwa ya kibinadamu katika nchi yote ya Afrika.

Nchi ya Sudan ya Kusini pamoja na ongezeko la vita vya wenyewe kwa wenyewe, ni vita vilivyo anza mwaka 2013 na kusababisha maelfu ya watu kufa na pia balaa la njaa.Migogoro hiyo imesababisha uvunaji mdogo wa mazao na kuathirika kwa kilimo.Ni nchi iliyo jitangazia uhuru wake 2011 ambayo pia yenye miogogoro mkubwa wa kiuchumi,mfumko wa bei umezidi asilimia 800% na wakati wa mijini wanakabiliana  na ongezeko la bei za bidhaa za vyakula.Inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 4.9 ya watu milioni 11 wana haja kubwa,mara moja, kwa misaada ya kibinadamu. Tarehe 20 Februari, serikali imetangaza hali ya njaa katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Ujumbe wa hivi karibuni wa Baraza la maaskofu kwa waamini wa Sudan ya Kusini unasema ya kwamba nchi iko katika mtego wa migogoro ya kibinadamu njaa,ukosefu wa usalama na maafa ya kiuchumi,hakuna shaka ya kwamba njaa imesababishwa na mtu.Ni kweli kwamba ukame umeathiri maeneo mbalimbali ya nchi nyingi , lakini ukosefu wa chakula kwa nchi yao umetokana na ukosefu wa usalama na usimamizi mbovu wa uchumi, aidha katika ujumbe wao wanasema Kanisa sio kupinga mtu yoyote na wala kwa serikali au upinzani.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.