“Nchi za Magharibi hawakuwahi kuwa na mawazo ya kuuliza Waafrika wanataka nini.Huo
ni ukoloni mamboleo.Ni utamaduni wa ubeberu , ni udikteta wa wafadhili matajiri” Huo
ni ujumbe unaonekana katika Video ya Obianuju Ekeocha Rais wa Utamaduni wa maisha
ya Afrika, ambao umeonekana hivi karibuni kwa kupinga maandalizi ya mkutano wa tarehe
2 Mach 2017 huko Brussels unao husu ufadhili wa kutoa mimba.
Mkutano huo wenye kauli “Yeye anachagua”umeandaliwa na nchi nne za Ulaya ikiwa ni
Belgium, Denmark, Uholanzi na Sweden.Ni mkutano wenye lengo la kukusanya fedha kwa
ajili ya utoaji mimba katika nchi zinazoendelea ,mara baada ya Marekani pamoja na
kuanzishwa sera mpya ya mji wa Mexico, ambao wanatoa kiasi kikubwa cha ufadhili kwa
mashirika yanayotoa huduma za utoaji mimba nje ya nchi.
Hata umoja wa Ulaya utakuwa na wawakilishi katika mkutano huo.Shirika la habari la
SIR limemnukuu Maria Hildingsson, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Kifamilia
Katoliki (Fafce),vinavyo jihusisha juu ya mahusiano ya afya ya uzazi ambapo pia uingia
hata kipengele cha utoaji mimba ,akisema “hiyo siyo sehemu ya Umoja wa nchi za Ulaya
kutoa utatuzi kama ilivyokuwa imetolewa mwezi Desemba 2013.
“Kuna sauti nyingi za waafrika na Ulaya wana omba msaada wa kuboresha usalama wakati
wa kujifungua na kusaidia afya ya uzazi , lakini si kwa ajili ya utoaji mimba”, anasema
Hildigsson,nakuongeza akikimbusha juu milioni mbili za saini zilizoanzishwa kwa ajili
ya maombi yao katika Tume ili wasitishe kutoa fedha za msaada unaojihusisha na utoaji
wa mimba.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |