2017-02-28 13:29:00

Ni vema kujua mizizi ya urithi wa utamaduni wetu na kuuthamini


Kuanzisha mjadala wa kimaadili kati ya wataalam wa Kanisa na Walei wa dunia kwa masuala ya dini,ili kutafuta mbinu sahihi zaidi yenye fursa ya kujua na  kujifunza kwa kina katika kutoa thamani ya urithi wa utamaduni wa kidini wa taifa, ambao ni vema kurithisha kizazi kijacho. Hiyo ndiyo lengo la Mkutano wa kitaifa wenye kauli mbiu “urithi wa utamaduni wa dini katika kuutambua,kuutunza na kuuthamini". Ni mkutano ulio andaliwa na Chuo cha Elimu ya kisayansi ya kiteolojia cha Mtakatifu Maria Di Monte Berico cha Vicenza Italia, wakishirikiana na Chuo Kikuu cha Kiteolojia cha Kipapa Marianum, pamoja na Taasisisi nyingine za Elimu ya Kisayansi ya dini unaotarajiwa kufanyika huko Verona nchini Italia tarehe 9 hadi 11 Machi 2017.

Kwa mujibu wa waandaji wanasema,  kujua vema mizizi ya urithi wa utamaduni wetu ni jambo  msingi wa kuweza kujua kuthamini kwa undani zaidi urithi tulio upokea na baadaye kuweza kuhifadhi kwa lengo la kuukuza kwa kipindi chote cha kihistoria ambacho katika ngazi ya kitaifa na kimataifa urithi huu unatoa sura ya kuharibiwa na kuathiriwa kwa kiasi cha kuleta hasara.Taarifa zinasema pia lengo la mkutano huo ni kuimarisha mafundisho ya Mtaguso wa Pili wa Vatican unaosisitiza juu ya thamani ya mazungumzo kati ya imani, liturjia, sanaa na usanifu kama msingi wa utamaduni  ambao unakumbatia miongo ya historia na  dini ya utamaduni ambao umeweza kuonekana katika maendeleo kuanzia Magharibi kuelekea Mashariki.

Kwa maana hiyo mkutano utakusanya wataalamu kutoka katika sekta mbalimbali wenye kuwa na ujuzi na  mbinu ya ufundishaji ili kuweza kutafakari juu ya historia , kisanii, na sanaa takatifu katika kuheshimu maudhui yake ya kiteolojia, na mwishowe  ili kubaini njia sahihi zaidi ya kujifunza, kuhifadhi na kukuza urithi huu mkubwa katika kuchunguza  kwa upya jukumu la diplomasia ya utamaduni.Waandaaji wa mkutano huo wanatoa ufungua  wa maeneo matano yanayo kusudiwa wakati wa siku hizo za mkutano huko Verona ya kwamba, watajikita katika sehemu ya sanaa takatifu na usanii wake, mandhari na maeneo ya imani,thamani ya urithi wa utamaduni wa dini,matukio ya hija , utunzaji wa urithi wa dini na dhidi ya kuzuia dharura. 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.