Hakuna kinacho halalisha ukatili dhidi ya wageni ,ni maneno ambayo yametamkwa na
Askofu Abel Gabuza wa Jimbo la Kimberly na Rais wa Kamati ya Haki na Amani ya Baraza
la Maaskofu wa Afrika ya Kusini (SACBC) wakati wa mkesha wa siku ya maandamo dhidi
ya uwepo wa wageni nchini Afrika ya Kusini ,maandamano yaliyofanyika Pretoria tarehe
24 Februari 2017.
Askofu Gabuza aliwataka waandamanaji wawe na utulivu na kujizuia , lakini ombi lake
halikusikilizwa kwasababu kumetokea mashambulizi ya wafanya biashara na wahamiaji
kwa mapigano na polisi ambao waliwatìa mbaroni watu zaidi ya 130.
Wahamiaji halali na wasio kuwa na vibali vya kukaa wanatuhumumiwa kuhusika na vitendo
vya uhalifu vinavyo kithiri na pia watu mahalia kulalamika kwamba ukosefu mkubwa wa
ajira nchini Afrika unasabaishwa na wageni hao.
Kwa njia hiyo Askofu Gabuza anasema"hatuwezi kukubali kesi za namna hiyo pamoja na
kusema eti kuna wageni wahalifu,jamii haiwezekani kujichukulia hatua za kisheria
mikononi mwao wenyewe, hivyo Askofu ameomba mashirika ya diaspora ya Afrika na polisi
kubaini wanao fanya vitendo vya jinai na uhalifu miongoni mwa wahamiaji waliopo na
hasa wale wanaoshiriki kuuza dawa za kulevya na ukahaba.Ameitka vilevile Serikali
kuimarisha uthibiti katika mipaka.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |