2017-02-27 15:35:00

Mapambano dhidi ya biashara haramu na madawa ya kulevya Bissau



Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio kwa upya juu ya Umoja wa Mataifa kuendelea na opereshi yake  nchini Guinea Bissau (Uniogbis),iliyo anza tangu mwaka 2009 katika nia ya kuunga mkono jitihada za kuleta utulivu wa nchi.
Kuhusu mpango wa Italia ambao wamekuwapo katika bodi ya mkutano wa usalama tangu Mosi Januari 2017,unaonesha kwa maandishi juu ya umuhimu wa kupambana na biashara haramu, hususani usafirishaji wa binadamu ndani na nje ya nchi na kupambana na vitendo vya jinai kimataifa ambavyo ni tishio la ukosefu wa utulivu wa nchi ya Guinea Bissau na mikoa yake.
Azimio lililotolewa katika maandishi linasema wanatia moyo katika juhudi zilizofanywa kwa mwelekeo wa serikali ya nchi pia wale wa Jumuiya ya kiuchumi katika nchi za Afrika ya Magharibi(ECOWAS,vilevile na wale operesheni ya Umoja wa Mataifa ,ikiwemo ile ya Ofisi za Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuthibiti madawa ya kulevya na uhalifu (Unodc).Halikadhalika ujumbe unathibitisha ya kuwa  ulanguzi haramu unao  tokea katika nchi za Afrika Magharibi unaathiri vibaya  nchi za Ulaya kupitia njia za bahari ya Meditranea.

Pamoja na habari hiyo,bado wakimbizi na wahamiaji wandelea kufurika katika visiwa vya Italia kwa kuokolewa na Meli za ukombozi.Hivi karibuni Meli ya ukombozi ya Norway imeokoa watu zaidi ya 993,  wakiwa wanaume 657, wanawake 100 na watoto wadogo 136, pamoja na meli nyingine ya Shirika lisilo la kiserikali imeokoa wakimbiz wengine 337 , wakiwa wanaume 248 , wanawake 16 watoto 71 kutokea nchi ya Guinea Conakry, Mali , Ivory Coast, Camerun, Ghana, Liberia,Togo, Senegal na Guinea Bissau.Taarifa zinasema kwamba hivi karibuni watu walikuwa wamepungua, ambapo hawakufikia zaidi ya elfu moja,lakini sasa wamerudia idadi kuongezeka kupita njia hizi za Italia, kwa ujumla operesheni  imeokoa watu 1700 katika bahari ya meditarenia katika njia kutokea Libia kwenda Italia .

Kwa mujibu wa Shirika la wahamiaji duniani  (OIM), wanasema,kwa miezi miwili sasa watu 366 wamesha poteza maisha yao katika bahari ya Meditranea.Kwa mwaka jana kipindi kama hicho japokuwa ulikuwa ni mwaka wa kutisha kwa wahamiaji, lakini ni  watu 97 tu walikuwa wamepoteza maisha.Halikadhalika Ripoti za takwimu za watu walio poteza maisha  kutoka katika Shirika la wahamiaji , linakadiria ni watu 326 kuanzia mwezi Januari kufikia 22 Februari mwaka huu, na kwamba kuna ongezeko la asilimia 100% kulinganisha na kipindi kama hicho mwaka 2016.Kwa upande mwingine takwimu za Shirika la kimataifa la uhamiaji (OIM) linaripoti kuwa, tangu mwanzo wa mwaka hadi sasa nchi za Ulaya wamefika  wakimbizi 13,924 kupitia njia ya Bahari  na kati yao asilimia 75% sawa na wakimbizi 10.701 wamepiga nanga nchini Italia na wengine wako Ugiriki na Hispania

Na zaidi nchini Italia kuna ongezeko kubwa kulinganishwa na mwaka 2016 wakati miezi miwili ya kwanza, taarifa zilionesha kutua kwa wahamiaji karibia 8100.Pamoja na hayo baada ya mwaka mmoja wa opereshini ya kituo cha Europol juu ya biashara ya binadamu ,imetangaza kwamba kuna upungufu wa biashara hizi kwa mashirikia yanayo jihusisha na biashara  za jinai  kwa mwaka 2016, sambamba na upungufu wa wanaoingia Ulaya bila uhalali.Pungufu ni wa takribani ya Euro bilioni mbili ukilinganishwa na mwaka 2015 ambapo kulikuwa na kadirio la faida kati ya euro bilioni 4,7 na 5,7.Kwa mujibu wa Europol inasema kuwa  wanaendelea kujikita ndani ya mitandao ya kijamii ambayo ndiyo njia inayo pendelewa zaidi na wahalifu wa biashara ya binadamu kupata upenyo katika kukuza na kuhamasisha uhalifu wao katika nchi zao mahalia.Utakuta wanatangaza zabuni za mambo kadhaa kama vile marazi, nyaraka za uongo ,vitambulisho, ruhusa na mawasiliano katika nchi.Hali kadhalika wanasema haikosekani  pia mashirika yanayotoa ahadi za vibali vya ndoa,ufadhili katika utafiti, masomo au kazi.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.