Ni furaha kukutana nanyi baada ya semina yenu wa mafunzo iliyo andaliwa na maakama ya Kanisa la Roma kuhusu mchakato wa talaka za ndoa.Namshukuru Decano na msaidizi kwa shughuli juu ya semina ya mafunzo haya.Kama ilivyo kuwa imejadiliwa na mapendekezo ya Sinodi ya Maaskofu juu ya mada ya Ndoa na Familia imeeleweka na kuanza kutekelezwa na pia kujumuishwa kwa njia ya hai kupitia wosia wa kitume upendo wa furaha,na pia kwa kutafsisiriwa katika sheria sahii za kisheria zilizomo katika hatua mbili yaani ya hiari yake mwenyewe na hiari ya huruma ya Yesu mwenyewe.Ni utangulizi wa Baba Mtakatifu katika hotuba yake mjini Vatican tarehe 25Februari 2017, kwa maparoko kutoka nje na ndani ya Italia kuudhulia semina ya mafunzo kuhusu talaka ya ndoa na familia .Baba Mtakatifu Francisko anasema ni jambo jema ya kwamba ninyi maparoko, kwa kupitia juhudi hizi za utafiti,mnaweza kufanya utafiti katika suala hili kwa kina kwa sababu ni nyinyi wahusika wa kuthibiti kwa hakika kila siku mnawasiliana na familia hizo.Sehemu kubwa ya kesi ni nyinyi wa kwanza kuulizwa na vijana ambao wanataka kuunda familia mpya kwa kuoa na kuolewa katika sakramenti ya ndoa.
Ni ninyi mnao kimbiliwa na wana ndoa kutokana na matatizo yao makubwa katika uhusiano
wao, katika migogoro hiyo wanataka kufufua imani na kugundua njia,ya Sakaramenti ,na
katika kesi kama hizi mara nyinyi wanataka maelekezo ya kuanza mchakato wa talaka.Hakuna
mtu yoyote zaidi kuliko ninyi anaye wajua hao na ambaye anawasiliana na kukabiliana
hali hali ya masuala ya kijami katika eneo hilo.Ni kwa uzoefu mbalimbali kama vile
sherehe za ndoa katika Kristo,ndoa sugu, ndoa za kiserikali,au kushindwa kwa ndoa,
familia na vijana wenye furaha na wasio na furaha.Kila mmoja katika hali hii ninyi
mnaitwa kuwasindikiza katika safari kwa kuhudumia na kuwapa msaada.
Awali ya yote katika kutoa ushuhuda wenu na neema ya Sakramenti ya ndoa ,na kuweka
kipaumbele wema wa familia,ambayo ni kiini muhimu cha Kanisa na jamii wakati wa kutangaza
kwamba ndoa kati ya mume na mke ni ishara ya umoja na utashi kati ya Kristo na Kanisa.Ushuhuda
huu unakamilika kutokana na maandalizi ya wachumba kwa ajili ya ndoa waweze kutambua
maana na kwa kina hatua ambazo wanatarajia katika safari yao ya maisha.Hali kadhalika
wakati mkiwasindikiza vijana , wasaidieni waishi katika mwanga na hata katika vivuli
,wakati wa furaha na hata katika majaribu , katika nguvu ya Mungu na uzuri wa ndoa
yao.
Msisahau daima kuwakumbusha wana ndoa wakristo ya kwamba katika ndoa Mungu anaangaza
na kujionesha sura yake , tabia yake isiyo futika ya upendo wake. Ndoa ni picha ya
Mungu,aliyo umba kwaajili yetu, na ambayo inaungana kwa dhati katika utatu mtakatifu
wa Baba Mwana na Roho Mtakatifu. Upendo wa Mungu katika utatu , upendo kati ya kristo
na Kanisa lake mchumba wake , unapaswa kuwa kiini msingi cha katekisimu na katika
unjilishaji wa ndoa.Kwa njia ya mikutano binafsi na katika jumuiya , katika mipango
na bila mipango, msichoke kuonesha kwa watu wote , hasa wana ndoa ,mafumbo haya makubwa.
(Taz. Ef 5,32).
Mkiwa mnatoa ushuhuda huo , ni wajibu wenu kuwasaidia hata wale wale ambao wamebaini
ya kwamba muungano wao siyo sakramenti ya kweli ya ndoa na wanataka kubadilika kutoka
katika hali hii.Katika kazi hii nyeti ni muhimu kuifanya kwa makini kwa namna ya kwamba
waamini wenu wawatambue siyo kwamba ninyi ni wataalamu katika vitendo vya urasimu
au kanuni za sheria , bali kuifanya kama ndugu wanaojiweka katika hali ya mtazamo
wa kusikiliza na uelewa.
Wakati huo huo , mfanye kwa njia ya Injili yenyewe , katka kukutana , kuwakaribisha
hata wale vijana ambao wanataka kuishi uchumba sugu bila kufumga ndoa. Wao katika
nazi ya kiroho na kimaadili ni miongoni mwa masikini na wadogo , ambao Kanisa katika
nyayo za Mwalimu na Bwana , Kanisa linataka kuwa mama ambaye hawezi kumtupa bali ni
kutafuta mbinu za kumkaribia na kumtunza .
Hata watu hawa wako rohoni mwake Yesu Kristo. Waangalieni kwa macho ya huruma , ni
huduma ya wali wanyonge na ni wa mwsho ambao Yesu anataja katika Injili , ni sehemu
muhimu ya huduma yenu kwa ajili ya kukuza na kulinda Sakramenti ya ndoa.
Mwenye heri Paulo wa VI alikuwa akifundisha ya kwamba Parokia ni uwepo wa Kristo katika
ukamilifu wa kuokoa kazi yake, ni nyumba ya Injili , ni nyumba ya ukweli , ni shule
ya Bwana wetu. (mafundisho ya Papa Paulo VI ”8 Machi 1964)
Baba Mtakatifu anaongeza ,nikiongea hivi karibuni na mahakimu wa Kanisa wa Roma ,
nilitoa pendekezo ya kuanzisha kweli njia ya ukatekumeni endelevu wa ndoa , ambao
unafunika hatua zote za kisakramenti kama vile kipindi cha mandalizi ya ndoa, maadhimisho
ya ndoa , na hata miaka itakayofuata,na hasa ninyi Maparoko ni wajibu kwa kushirikiana
na maaskofu , ambao wamewakabidhi kazi ya ukatekumeni .Ninawatia moyo japokuwa ni
ngumu ambayo mnakutana nayo.
Namshukuru kwa uwajibikaji wenu kwa ajili ya ya kutangaza Injili ya familia. Roho
Mtakatifu hawasaidie kuwa wahudumu wa amani na furaha katikati ya watu watakatifu
waaminifu wa Mungu, hasa kwa watu wanaoishi katika mazingira magumu na masikini katika
huduma yenu ya kichungaji.
Wakati huo naomba sala kwajili yangu na ninawapatia baraka kila mmoja wenu na jumuiya
zenu za kiparokia.
Sr Angela Rwezaual
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |