2017-02-24 13:20:00

Jitahidini kuwa ni watu wenye haki na huruma kwa jirani!


Katika safari ya mkristo , ukweli hauna majadiliano, bali wewe unatakiwa kuwa mwenye haki na huruma kama alivyotufundisha Yesu, ni maneno ya Baba Mtakatifu Franciko katika misa yake ya asubuhi ya tarehe 24 Februari katika Kikanisa cha mtakatifu Petro Mjini vatican, akiwaonya waamini juu ya ubinafsi  na kudanyanyika kwa imani finyu katika mantiki ya kushukilia tu katika  kupambanuna mema na mabaya. Ni haki kumpa talaka mke wako, hilo ni swali kutoka katika Injili ya Mtakatifu Marko, ambapo walimu wa sheria waliuliza Yesu akiwa anahubiri watu katika eneo ya Yudea.Yesu  hababaishwi na mantiki ya elimu ya kupambanua na hivyo anawaelezea ukweli .Wanafanya hivyo kwa mkumjaribu mara nyingine tena , japokuwa katika jibu la Yesu linatoa nafasi ya kuwaeleza ni jambo gani la msingi katika imani.


Yesu hawajibu kama hairuhusiwi na wala inaruhusiwa , yeye haingilii kwenye  mantiki zao za elimu ya kupambanua mema na mabaya kwasababu wao walifikiria tu , juu ya imani ya kwamba unaweza ua huwezi , kwamba kuna mahali unaweza kufikia na mahali huweza kufikia, yaani hiyo mantiki ya kupambanua . Kutokana na kutokuingilia elimu yao, ndipo Yesu anatoa swali  juu ya  Musa aliwaagiza nini katika sheria yenu?Jibu lao ni kwamba wameruhusiwa kutoa talaka, na kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anasema wao wenyewe wanajiingiza katika mtego .Kwa sababu hiyo Yesu anawaleza jinsi gani walikua wagumu wa moyo ,kwani hiyo sheria aliwaandikia wao inasema ukweli , haina kuchangua , hai kuomba ruhusa , ni ukweli.


Yesu daima anasema ukweli , anaeleza mambo jinsi yalivyo, anaongeza Baba Mtakatifu ,ukweli wa maandishi  ya sheria ya Musa .Hiyo pia aliwaelezea hata mitume wake, mbele ya tukio la mwanamke mzinzi , ya kwamba anaye mpatia talaka mke waka akaoa mwingine , anatenda dhambi naye , na hata kama mke amemwacha mme wake akaolewa na mwingine , naye anazini. Lakini kama ukweli ndiyo huo, uzinzi ni  hatari , na je unaweza kuelezea namna gani kwani Yesu mara nyingi ameweza kuongea  na  mzinzi, mpagani , na alikunywa katika glasi yake , ambayo ilikuwa haijasafishwa? na pia alimwambia mwanamke  mimi sikuhukumu , bali usitende dhambi tena!Je, ni namna gani ya kuelezea hilo? 

Njia ya Yesu ni wazi , ni njia ya kutenga wema na ubaya katika ukweli na katika huruma. Baba Mtakatifu Francisko anatoa jibu. Yesu anawaacha nje wale ambao wanataka kumweka majaribu ya kutaka kupembua na kueleza mema au mabaya . Ambapo katika sehemu nyingine ya Injili aliweza kuwambia nyinyi ni wanafiki . Kwa njia hiyo hata amri ya Mungu ya nne hawa walikuwa wanafikiria wamewapa  wazazi msaada wa Kanisa . Ni wanafiki, maana upembuzi wa kuchanganua mema na mabaya uliwafanya kila wakati kusema hiki unaweza na kile huwezi , na kwa taratibu ugeuka kuwa ufunyi  na mwisho kuwa shetani, kwasababu ya kuweka vizingiti vya  kuanzia  hapa unaweza ,hadi hapa huwezi hiyo ni udanganyifu wa elimu ya kuchangua wema na ubaya.

Taadhali ya Baba Mtakatifu anasmea,safari ya mkristo daima isiangukie katika mantiki  ya kupembua , bali inabidi kujibu ukweli ambao unatusindikiza , kwa mfano wa Yesu katika huruma , kwasababu yeye alitolewa na mwanadamu kwa njia ya huruma ya Baba , na kwa njia hiyo yeye hawezi kukanusha mwenyewe.Hawezi kujikanusha mwenyewe  kwasababu ni ukweli wa Baba , na huwezi kujikanunusha mwenyewe kwani ni huruma ya Baba. Hii ndiyo njia ambaya Yesu anatufundisha, ni ngumu katika utekelezaji mbele ya vishawishi vya ukweli.

Hali kadhalika Baba mtakatifu anapembua ya kwamba tunaposhikwa na kishawishi katika mioyo yetu , safari ya kuondokana na elimu ya kuchanganua mema na mabaya  katika ukweli na katika huruma , huonekana siyo rahisi. Inahitaji neema ya Mungu ili atusaidie kwenda mbele .Tunapaswa kuomba daima kwa Bwana ya kwamba tuwe wenye haki na huruma , kama yeye mwenyewe , na kuwa na utambuzi wa kujua ni jambo gani lenye maana,kwasababu siyo mambo mawili bali ni jambo moja tu. Mungu ni wa haki na wa huruma , ni wa huruma na haki.Bwana aweze kufanya tuelewe njia hii ambayo siyo rahisi , lakini itafutanya kuwa wenye furaha binafsi na kwa  wengine.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.