Ili wahamiaji wapate kubadilika na kuhitahiji fursa , amani na maendeleo ya pamoja katika familia ya binadamu.Ni matashi mema ya Katibu Mkuu wa Vatican Petro Parolin wakati wa hotuba yake Jumatano 22 Februari 2017 kwenye Jukwaa la VI la Kimataifa juu ya Wahamiaja na Amani kwa kaulimbiu “ushirikishwaji na maendeleo: kuanzia mwanzo hadi kufikia matendo”.Jukwaa hili limeandaliwa na Baraza la kipapa la Vatican la maendeleoo na binadamu,Mtandao wa Kimataifa wa Shirika la Scaribian kwa wahamiaji na Chama cha Konrad Adenauer.
Kardinali Pietro Parolin anakumbusha juu ya Baba Mtakatifu Francisko anavyotia moyo
kila anapopata fursa na kuwataka wote kuchukulia hatua ya matukio haya ya wahamiaji
, ambayo ni mojawapo ya matatizo ya msingi katika ulimwengu wa sasa.Katika ulimwengu
wa sasa , ambao unatawaliwa na utandawazi ,unahitaji nguvu ya pamoja katika kuonesha
jinsi gani amani , maendeleo na kuheshimu haki msingi za binadamu inawezakana kwasababu
kwa sasa imeanza kuonekana ishara msingi katika juhudi kwa maana ya mahusiano kati
ya nchi na kati ya watu.
Kardinali anayataja matatatizo mbalimbali na mengi kama changamoto ya sasa akisema
ni pamoja na sera za kisiasa kupenda kujinufaisha kwa riba na pia ishara ya hofu ya
siasa za kutatanisha mipango,vilevile maendeleo ya chini na mageuzi ya matumizi ya
fedha,na lengo la kuondokana migogoro isiyo kuwa na mwisho, ukiukwaji wa haki za binadamu,
wasiwasi wa madhala ya mabadiliko ya tabianchi, na migogoro ya kiuchumi hayajatatuliwa
, suala la itikadi kali pia misaada ya kibinadamu,kuzorota kwa kisiasa,kijamii,kibinadamu,kimazingira,
na biashara ya jinai ya watu.Haya ni baadhi ya mambo yanayosabisha uhamiaji na zaidi
pia kuwa vikwanzo na belia kwa upande wa siasa ya wahamiaji, kuongeza njia mbadala
na zaidi ni hatari kwa wahamiaji wasio kuwa na vibali kuingia mikononi mwa unyonyaji
na unyanyasaji kwa upande wa watu wahalifu, na kusabisha maisha ya binadamu kupotea.
Karidinali Pietro Parolin anaongeza pamoja na uhalifu huu, bado kuongezeka tena
matatizo mengine ya wahamiaji ambayo yanakuwa mizigo katika nchi nyingine,mahali ambapo
uchumi na siasa huko hatarini, na ambapo nchi hizo haziwezi kukabiliana au kuhakikisha
haki msingi za watu, au kulinda heshima ya utu wao vinatekelezwa.Pamoja na hayo pia
Kardinali anasema uhamiaji kimataifa , haiwezi kufikirika kwamba ni dharura ya mpito
tu , bali ni haki ya binadamu ya kuwalinda,na ni chombo ambacho kinapaswa kutazama
kwa ujumla katika bara na kukabiliana na sababu zake kwa kutafuta mikakati ikiwemo
ushirikiano kwa upeo wa pamoja kiulimwengu kwani anasema "ipo haja ya ushirikiano
katika ngazi zote, kutokana na uchunguzi wa matatizo ya sasa na mapungufu ya kila
nchi kwa kukabiliana peke yake na changamoto hii kubwa kwa jumuiya ya kimataifa kwamba,
katika nafasi ya kwanza, lazima lengo la kuhakikisha watu na amani ya mtu binafsi
na maendeleo, katika kufanya uhamiaji unakuwa ni chagua badala ya kuwa lazima.
Kwa ujumla Kardinali Pietro Parolin anahitimisha hotuba yake akisema ni lazima kujikita
katika uchumi umoja ambao unajenga maisha kwasababu unashirikisha masikini, hutumia
faida katika kujenga umoja,na unaweza kuleta matumaini katika ulimwengu ambapo pia
ni njia ya kukutana,na kuleta matumaini mapya,heshima,utajiri wa mahusiano ambapo
hata fedha kwa mtazamo wa kubadilishana zawadi,unaingia kaitka mzunguko wa mara mia
kama ilivyotajwa hata katika Injili na kwamba "kwa yule anaye toa na anayepokea"ili
furaha iweze kuwa kwa wote.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |