2017-02-21 15:58:00

Tuepuke tamaa ya kupenda ukubwa bali kuiga mfano wa kutoa huduma


Bwana anatupatia neema ya haibu takatifu mbele ya vishawishi vinavyo tugusa wote hata katika Jumuiya ya Kanisa , ni maombi ya Baba Mtakatifu Francisko katika Mahubiri yake Jumanne 21 Februari 2017 katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vatican, Baba Mtakatifu anakumbusha wito wa Yesu kwa mitume katika kujikita katika uhuduma kwa wote. Akitafakari kutoka somo la Injili ya siku, Baba Mtakatifu anasema wote tunashawishika, akikimbusha namna ya kutoa huduma kwa Bwana  kama Yesu alivyo wasimulia mitume wake juu ya kifo chake, lakini wao hawakuelewa , wakawa na hofu ya kuuliza nini maana yake. Hii ni kishawishi, cha kutokuwajibika: pamoja na hayo hata Yesu  alijaribiwa kwanza jangwani mara tatu na shetani , baadaye na Petro mara baada ya kuwaelezea juu ya ujio wa kifo chake.

Anaongeza akisema pamoja na hayo bado kuna kishawishi kingine kama Injili inavyoeleza juu ya mitume wake kubishana nani atakuwa mkubwa , na Yesu alipo wauliza wanajadili nini,wote walibaki kimya kwa aibu ya kile walicho bishania. Hawa ni watu walio kuwa wema na walikuwa wanataka kumfuata na kuhudumia Yesu , japokuwa hawakuwa na utambuzi ya kwamba njia hai  ya kufuata Bwana si rahisi  na siyo kama vile ya  kuzunguka katika chama cha hisani , ukitenda vizuri, hapana, kumfuata Yesu ni jambo jingine!.Mitume walikuwa na hofu , lakini pia  wakawa na vishawishi vya kiulimwengu , kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anabainisha kuwa tangu mwanzo wa Kanisa hadi leo ni tabia inayo endelea kujitokeza.Katika hilo anatoa mfano wa kutazama ndani ya maporokia, ni mapambano mangapi ya kusikia huyo akisema mimi ninataka kuwa mwenyekiti wa chama, au kusikia nani mkubwa katika parokia hii?Majibu ni kwamba Baba Mtakatifu anasema "mimi ni muhimu kwasababu ya mengi niliyotenda , yule haiwezekani, kwasababu ya yale yote aliyotenda … kwa namna hiyo, ni kuvalisha minyororo ya dhambi.

Kwa kishawishi hicho upelekea maseng'enyo kwa wengine.Mifano mingine hai  ili kutambua kishawishi hiki anasema “ mara kwa mara  hata wakleli kwa aibu wanasema , mimi natamani parokia ile, lakini  Bwana yuko pale….Hiyo siyo njia ya Bwana bali ni njia ya ubatili wa kiulimwengu anasema Baba Mtakatifu. Hata kati ya Maaskofu mambo hayo yanatokea ya kutazama jimbo lipi ni muhimu na kuwa na kishawishi au tamaa ya kutaka kufanya kama wengine.Tamaa  ya kuwa mtu  wa maana inatusukuma kuelekea njia za kiumwengu . Baba Mtakatifu Francisko anasema ni kuomba kwa Bwana , neema ya kuwa na aibu tunapojikuta katika hali hii.Kwasababu Yesu mwenyewe anabadili mantiki hiyo kwa dhati akiwakimbusha kwamba yeyote anayetaka kuwa wa kwanza , awe wa mwisho kuhudumia wote kuwaonesha mfano wa  mtoto mdogo kati yako.


Vilevile Baba Mtakatifu anawataka wasali kwa ajili ya Kanisa na kwa ajili ya wote ili Bwana atukinge na zile tamaa za kupenda malimwengu na ya kujisikia wakubwa zaidi ya wengine. Na zaidi kuwa na neema  ya kuwa rahisi kama wa mtoto wadogo wanao tambua njia pekee ya kufuata katika kutoa huduma. 

Angela Rweazaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.