Injili ya Jumapili kutoka (Mt 5,38-48) ni kurasa ambazo zinajieleza vema kuhusu mapinduzi ya kikristo,kwani Yesu anaonesha njia ya haki ya kweli ya kwamba upendo uzidi sheria ya mkato wa ncha kali, yaani jicho kwa jicho na jino kwa jino.Sheria ya zamani ilikuwa kama vile ya kulipiza kisasi, adhabu ya kifo aliye kuwa ameua au kukatwa miguu aliyekuwa amedhulu mwingine.Yesu hataki mitume wake wapokee mabaya, bali nia yake ni kwamba nao waingilie kati bila kufanya ubaya wowote kujibu vibaya, siyo kuvunja mnyororo wa ubaya, ni sawasawa na kuendeleza ubaya huo.
Ni tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko aliyoitoa Jumapili 20 Februari 2017 kwenye
uwanja wa Kanisa kuu Mtakatifu Petro mjini Vatican wakati wa sala ya Malaika wa Bwana.Baba
Mtakakatifu anaonya kulipiza kisasi bali kujaribu kukwepa visasi hivyo ikiwa njia
ya ukristo wa kweli. Anasema,iwapo kuna uwezekano wa kuvunja mnyororo wa ubaya ,
ni hakika kweli mabadiliko kuwapo.“ Ubaya kwa hakika ni utupu na haiwezekani kujazwa
na utupu, bali kwa ujazo, maana yake kwa wema".Tabia ya kulipiza kisasi siyo soluhisho
la migogoro. Akitoa mfano, umenifanyia mabaya nawe utakiona! hiyo tabia haitatua matatizo,
na siyo tabia ya kikristo.
Kitendo cha Yesu kukataa vurugu ni njia ya kusema kwamba inahitajika haki halali,
akitoa mfano ya wa kugeuza shavu la pili, wa kutoa mavazi au kujitoa sadaka mwenyewe.
(Mt 5 39-42.).Lakini kujikatalia mambo hayo haina maana kwamba hakuna haja ya kufanya
haki isitendeke la hasha! ,kinyume chake ni upendo wa Mkristo unajionesha kwa namna
ya pekee ya huruma na kuwakilisha utambuzi mkubwa wa haki.
Yesu anataka kutufundisha njia sahihi ambayo tunatakiwa kufanya ya kutofautisha
haki na kulipiza kisasi.Kulipiza kisasi Baba Mtakatifu anasema kamwe siyo haki.Wajibu
wetu ni kufanya uadilifu wa kutafuta kutenda haki na kukatazwa kulipiza kisasi kwa
njia yoyote na hata kwa kuchochea kisasi kwa maana ni aina ya chuki na vurugu.
Yesu hataki kupendekeza utaratibu mpya wa serikali,badala yake ni amri,ambayo pia
ni pamoja na upendo kwa maadui wa mtu isemayo "wapendeni adui zenu na kuwaombea wale
wanaowadhulumu ninyi" (i44). Na hii si rahisi!.
Lakini Neno hili lisieleweke kama mhuri wa uovu unaofanywa na adui,bali kama mwaliko
na mtazamo wa upeo wa juu wa ukarimu sawa ule wa Baba Yetu aliye mbinguni, ambaye
Yesu anasema “huchomoza jua juu ya watu wabaya na wema,na uwanyeshea mvua wati wanyofu
na waovu"(45). Hata adui kiukweli ni binadamu aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu hata kama
sasa amefunikwa na kivuli cha maovu na kuonekana hastahili.
Tunaposema maadui, tusifikirie juu ya nani ambaye ni tofauti na kuwa mbali na sisi,
tunajadili kuhusu sisi wenyewe, ya kwamba tunaweza kuingia kwenye mgogoro na majirani
zetu,wakati mwingine pamoja na familia.Swali, ni maadui wangapi ndani ya familia,
tufikirie hilo! Baba Mtakatifu Francisko anatoa mifano mingine ya kwamba,maadui pia
ni wale wanaosema vibaya juu yetu, wanao wasingizia wengine, na kutufanya vibaya.Hiyo
si rahisi kumeza anadhibitisha .Kwa wote wanaitwa kukabiliana nao kwa wema , kwa maana
ni mojawapo ya mikakati inayo ongozwa na upendo.
Bikira Maria atusaidie kumfuata Yesu juu ya njia hii ngumu, ambayo dhati huongeza heshima ya binadamu na kutufanya kuishi kama watoto wa Baba yetu aliye mbinguni.Atusaidie kufanya mazoezi ya uvumilivu , mazungumzo , msamaha, na hivyo kuwa mafundi stadi wa umoja na ndugu zetu katika maisha yetu na hasa kuanzia ndani ya familia.
Baada ya sala ya malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu aliwahutibia mahaujaji
wote katika viwanja vya Mtakatifu Petro akisema:
Anasitikitishwa na habari zinazoendelea kutolewa za mapigano na vurugu na ukatili
katika Mkoa wa Kasai ya kati nchi ya Jamuhuri ya kideomkrasia ya Congo.anasema Baba
Mtakatifu kwamba anahisi maumivu makubwa kwa wathirika na hasa watoto wengi ambao
wametolewa kwa wazazi wao na katika shule, ili kwenda kutumika kama asikari. Hili
ni janga la watoto kuwa maaskari!
Anawakikishiwa ukaribu wake kwa maombi yake , hata kwa ajili ya wafanyakazi wa dini na mashirika yasiyo ya kiserikali ambao wanafanyaka kazi katika ukanda huo mgumu .Anarudia kwa upya kutoa wito wa dhamira kwa viongozi wa Taifa na kwa jumuiya za kimataifa , ili kuchukua maamuzi sahihi kwa wakati ili kusaidia ndugu wanaozidi kuteseka.
Halikadhalika Baba Mtakatifu anaomba kusali kwajili ya watu wote hata katika sehemu
nyingine za Bara ka Afrika na ulimwenguni wanaoteseka kwa sababu ya vurugu na vita.Akitaja
nchi ya Pakstan, Itaq ambao wanazidi kukumbwa na vitendo vya ukatili wa kigaidi siku
zilizopita.
Baadaye aliomba kubaki kimya kwa kitambo baadye sala ya salam Maria .
Alimazia akiwasalimia wote mahujaji kutoka sehemu mbalimbali za dunia na mwisho kuomba
sala kwa ajili yake .
All the contents on this site are copyrighted ©. |