Maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana kwa Mwezi Oktoba, 2018 yataongozwa
na kauli mbiu “Vijana, Imani na mang’amuzi ya Miito”.Maandaliz hayo yameanza kwanza
kutoa hati ya maandalizi ya Sinodi ya XV .Kwa maandalizi ya hati hiyo nikutaka kuangalia
vijana wote duniani katika utambulisho na ushiriki wao katika maisha yao binafsi .Pamoja
na taasisi katika mchakato wa kuunda vijana wa kizazi kipya.Tunaweza kusema ni ramani
zaidi kama tusomavyo kwenye utangulizi wa hati hiyo ambayo inajikita kwa undani zaidi
kwa vijana katika mang’amuzi ya.
Hali kadhalika hati hiyo inatazama kwa mapana shughuli za kichungaji kuhusu miito
na kuwataka viongozi wa Kanisa kufanya hija na vijana kuwasindikiza na hatimaye waweze
kugundua, kuona na kuitikia wito wa kumfuasa Kristo Yesu.Kwa njia hiyo ni dhahiri
kuona walengwa ni vijana wote pasipo kubagua na familia kama kiini cha miito , watu
ambao wawe mfano bora wa kuigwa.
Pia kuna katika hati hiyo bado inaonesha sekta ipi vijana wanapendelea hili Kanisa
liweze kushughulikia kikamilifu katika kazi ya kichungaji kwaaili ya miito.Sekta
hiyo ni katika mitandao ya kijamii ambap Kanisa linapaswa kujitahidi kuwakuta ili
kuwaongoza Vijana
Mwandishi wa habari za Radio vatican, alifanya mahojiana na Kardinali Lorenzo Baldisseri
Katibu mkuu wa Sinodi ya Maaskofu kuhusiana na hati hiyo ya maandalizi na kuchambua
kwamba , Sinodi hii ni kutaka kwa dhati kuwahusisha vijana kutokana na kwamba mara
nyingi kuna misemo inayo sikika , vijana ni wadhaifu,vijana ni wenye matatizo. Anasame
ni lazima kutambua ya kwamba vijana ndiyo mpango wa maisha endelevu na kwa hiyo ni
vijana wa maisha hata ya ya sasa. Ni wajibu wetu kutambua hilo, kuwapa fursa na
vipaumbele zaidi kama wahusika wakuu katika maisha yao ndani ya kamii.
Watu wazima ,hatulazimiki kuwapinga mawazo yao , bali mi muhimu kuwasindikiza , kuwatia
moyo, kuwashauri, kama kwa mfano “ tazama vijana maisha ni kuwajibika, ni kazi ,lakini
ni uzuri ni furaha, aidha tazama vijan, tunataka ya kwamba mtambue vema furaha ambazo
sisi tunawalekeza ni kutokana na uzoefu wetu,kwa utulivu pokeeni ili nanyi mpate kukubali
na kuwajibika katika kujenga maisha yenu ya leo na endelevu.
Hali kadhalika anasema ya kwamb Sinodi itawasikiliza vijana kwa ajili a kuwawezesha
uwezo wa kujieleza wao wenyewe na kubadilishana mawazo yao kwa wengine yale yatakayo
kuwa maisha yao endelevu.Katika Hati ya maandalizi kuna kipengele ambacho kinaleza
juu ya njia zilizotumika zamani ya kwamba hazifanyi kazi tena, kwasababu uzoefu wa
kizazi kilichopita, kinaonekana kupitwa na wakati kwa haraka. Kwa njia hiyo inabidi
kutafuta mbinu mpya za kuwashirikisha vijana ,kitu ambacho kwa hakika Sinodi ya vijana
ndiyo kazi inayotakiwa kufanya.
Kardinali Baldisseri anasema kwa hakika Sinodi inataka kutafuta hawali ya yote
lugha ya kutumia kwaajili ya kuwasindikiza vijana.Lugha ambayo inawezesha vijana kuelewa
kwa haraka kutokana na mabadiliko ya kukua kwa kwa haraka kwani mara nyingi inakuwa
vigumu kueleweka kwa watu wazima,na kwa njia hiyo husababisha hukuma siziso na msingi
, hivyo mbinu zilizotumika za kizamani lazima kubadilishwa na kuweka mwendelezo wa
mbimu mpya ambayo itawezesha kueleweka kwa wote na kuifuata.
Kardinali pia anaelezea juu ya Sinodi hii kuwa na mitazamo ya wosia wa kitume wa “Furaha ya Injili” na “Furaha ya Upendo”na kusema katika wosia hiyo wito wa neno la vijana limetamkwa mara 36 , na kwa njia hiyo ni kupata kielelezo cha kuweza kueongelea mada hiyo kwa vijana . Ni dhahiri ya kwamba familia ndiyo msingi ambapo umeongelewa kwa miaka hii mitatu.Na kwasasa lakini mababa wa Sinodi wataongea mada ya vijana .Na hiyo ni hja kubwa ya kuengea mada hii kwasababu ya mwendelezo wa mada ya familia ambapo ndiyo umekuwa mpango wa Baba Mtakatifu Franciko.Kwa upande wa (Evangelii Gaudium) “Furaha ya Injili” tunakutana na mada zote , hati hizi mbili ni muhimu kwa ajili ya kuelewa zaidi kile kinachotendeka kwa sasa:na kwa njia hiyo maandalizi ya hati ya vijana italeta matokea mengine baadaye wakati ikifika muda wakufungua Sinodi hiyo.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |