2017-02-13 15:35:00

Askofu Mkuu H. Hoser ateuliwa kuwa Mwakilishi wa Papa Francisko.


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Mkuu wa Warsaw -Praga  nchini Uholanzi  Henryk Hoser, S.A.C. kuwa mwakilishi wake maalum huko Medjugorje nchi Bosnia. Nia ya Baba Mtakatifu kumtuma huko ni kuangalia mahitaji ya mahujaji wanao kwenda huko. Kutokana na wingi  wa watu hao , anakwenda kuona shughuli za uendeshaji wa shughuli za kichugaji na ikibidi kutoa ushauri kwaajili ya maendeleo endelevu ya shughuli za Kanisa katika  uchungaji.

Pamoja na ziara hiyo, Askofu  Mkuu Henryk Hoser, S.A.C. ataendelea  na shughuli zake za kichungaji katika Jimbo lake Kuu  Warsaw - Praga  wakati huo huo akiendelea pia na utume alio takiwa na Baba Mtakatifu hadi atakapomaliza utume huo wakati wa kiangazi mwaka huu.Ikimbukwe kwamba ni maelfu na maelfu ya watu wanaelekea katika eneo hilo kwaajili ya kusali katika Kanisa la Maria wa Medjugorje nchini Bosnia Ulaya ya Mashariki.

 

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya radio Vatican.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.