Ni miaka 88 ya mkataba wa Laterano kwasababu tarehe 11Februari 1929 Kanisa Katoliki
na Serikali ya Italia ,walitia saini a mkataba wa makubaliano ya masuala ya ushirikiano
katika utendaji wa shughuli za utume wa Kanisa. Vilevile mwaka huu unakwenda sambamba
na uhusiano muhimu wa tukio la ishara ya mwisho kuhusu mji wa Roma, kwa njia hiyo
ni tukio la upatanisho kati ya Kanisa na Serikali ya Italia ambapo ulikuwa ni uzinduzi
wa kushirikiano kati yao.
Kwanza inabidi kukumbuka sheria ya Kanisa kupitishwa ,ambayo ni ya kwanza katika historia
ya Kanisa kwa kupitia kazi ya mikono ya Papa Benedikto wa XV mwaka 1917.Ni sheria
iliyo anzishwa kwaajili ya kukidhi haja ya kiu katika ngazi ya kichungaji na Papa
Pio wa X kwaajili ya kusaidia Kanisa waingie bahari ya kisasa na kuunga mkono shughuli
za kichungaji kwenye kupiga makasia katika bahari mpya na ngumu.
Kwa mtazamo wa hatua za historai hiyo ni kwamba Sheria hiyo ilijitokeza wakati wa
kipindi ambacho Serikali ilikuwa imewatoa nje Kanisa wasiwe na haki ya sheria
katika mfumo wa raia,ki ukweli hali hiyo ilileta matatizo makubwa ya maisha ya Jumuiya
ya Kanisa , ambayo ilikuwa inaishi na inaitwa kuishi katika watu wa nchi hiyo ya Italia.
Halikadhalika Kanisa ilikuwa inajikita kutoa ishara kubwa na manufa ya wote kama
vile ukombozi kutokana na madai ya kale na sheria za kiserikali.Kwa njia hiyo Kanisa
liliweza kijipanga kisheria kutokana na uwezekano wa binadamu, kwa ajili yake , na
kuwa na haki katika katiba na uhusiano na mwisho kwa kila mtu.
Kwa muonekano zaidi tunaweza kusema kwamba sheria ilionesha ni muhimu kwa Kanisa walioitwa
kukukabiliana na upungufu wa demokrasia , na upinzani katika ujio wa udikteta kwa
wakati huo .Na katika hatua hii ni dhahiri kwamba makubaliano ya mkataba wa Lateran
,ilitokea wakati wa matukio ya nchi na kufungua mlango wa Porta Pia tarehe 20 Septemba
1870, kwa njia hiyo ilikuwa na matunda ya mkataba huo kwasababu nyuma kulikuwa tayari
kuna nyenzo za kisheria zimepagwa vizuri.
Maadhimisho ya pili ni yanahusiana na kuzaliwa kwa Jamhuri ya nchi ya Italia , baada
ya mwisho wa udikteta na vita.Kipndi hicho kilitawali na maadili ya juu na mawazo
motomoto licha ya kwamba kulikuwa na utofauti katika nafasi za kisiasa ambazo zilikuwa
zinafanya umoja wa Italia kuwa mgumu katika kutafuta ukombozi.
Kukumbuku hiyo ya Katiba ambayo ilipitishwa tarehe 22 Desemba 1947 ikaungwa mkono
na idadi kubwa ya watu na kuanza mara moja kwa kasi zake tarehe 1 Januari 1948.Katiba
hiyo kwa hakika inatoa kipengele katika haya ya pili Ibara ya 7 ambapo mkataba wa
Lateran , kwa dhati unathibitisha.Kwa mtazamo huo ni kushukuru kufanyika marekebisho
yalikuwa yamekubaliwa katika mkataba kwenye makao makuu ya serikali ya Italia Villa
Madama ya mwaka 1984. Mikataba hiyo imeweza kuendelea kukuana nguvu chanya zilizopo
katika vifungu vinavyo husika.
Lakini wito mkuu wa Katiba kwa mtazamo wa mahusiano yaliyopo kati ya Kanisa na Serikali
unaleta maana zaidi, kwasababu vipengele kadhaa kama vile nafasi ya maadili, juu ya
utaratibu wa sheria ya Italia na maadili ya kijamii ambayo ni kanuni ya pamoja na
wote,vilevile kuanzisha umuhimu wa binadamu na hali zake , utu wa binadamu , na
kanuni ya misingi ya mshikamano.
Halikadhalika katika uwanja wa matukio ya dini, uwepo wa uhuru shirikishi, kitaasisi
na uhuru wa raia bila ubaguzi , wakati huo kwaajili ya kushirikiana kati ya Kanisa
na Serikali ili kukuza wema wa binadamu kama isemavyo Katiba Ibara ya 1 ya mkataba
huo.
Aidha unahusu ushirikiano ambao ni alama ya miaka mingi bila kuwa na utata wa majukumu
na shughuli, katika kuhamasisha ukuaji wa nchi katika masuala ya zana na maadili,ambao
kwa mara nyingine tena ,umepata nafasi za kujieleza katika nchi kwa mantiki ya asili
ya mkataba ambao unaadhimishwa miaka 88 japokuwa katika uchungu wa matukio mbalimbali
yaliyo jiokeza hivi karibuni , na ambayo kwa kiasi kikubwa ni wa kusikitisha na kugusa
watu wengi Italia na pia kusikitishwa na maisha ya jumuiya nyingi kwa ujumla.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |