Kwa neema ya Yesu , itusaide tusifiche udhaifu na vishawishi vyetu tilivyo navyo
bali tuombe msaada wa kutuinua ili tuendelee mbele.Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko
katika mahubiri ya Ijamaa 10 Februari wakati wa Ibada ya Misa kwenye Kikanisa cha
Mtakatifu Marta Mjini Vatican.
Akitafakari mwendelezo wa somo la kwanza kutoka katika kitabu cha mwanzo , sehemu
ya ya shetani akiongea na mwanamke, ili aweze kuanguka katika dhambi kwa udanganyifu.Baba
Mtakatifu anasema, vishawishi hupelekea kujificha kwa Bwana na hivyo inakufanya kubaki
mwenya dhambi, na udanganyifu .
Katika vishawishi na dhambi Baba Mtakatifu anatazama somo kuhusu Adamu na Eva na pia
Maongezi ya Yesu na shetani jangwani, na kusema ni shetani anayeonekana kwa mfano
wa nyoka ,anatumia ushawishi kwa maneno ya ulaghai , kwa maana yeye ni mtaalam, na
ni baba wa wa uongo. Yeye anajua namna ya kulaghai, na jinsi gani ya kurubuni watu.
Yeye alifanya hivyo kwa Eva kwa uongo wake, akaanza mazungumzo naye , hatua kwa hatua
akampeleka mahali anapotaka yeye.
Kwa upande wa Yesu ni tofauti , anaeleza Baba Mtakatifu kwa sababu shetami alifika
mahali pabaya.Alitafuta namna ya kuzungumza na Yesu , kwasababu shetani daima anapata
kudanganya mtu kwa njia ya mazugumzo :anatafuta namna ya kundanganya , bali Yesu hakuweza
kuanguka katika udanganyofu huo. Kwa naana hiyo shetani anajieleza mwenyewe, lakini
Yesu pia anampatia jibu ambalo ni neno la Mungu. Kwa maana hiyo haitakiwi kabisa kufanya
mazungumzo na shetani, la sivyo unataishia kuwa kama Adamu na Eva walivyo fumbuka
macho na kuona utupu.
Shetani halipi vizuri, ni mdanganyifu, anatoa ahadi kwa yote na kukuacha utupu. Hata
hivyo Yesu mwenyewe alibaki utupu msalabani , si kwaajili ya shetano bali kwaajili
ya kumtii Baba yake, lakini hiyo ni njia nyingine.Nyoka ambaye ni shetani ni mjanja,
huwezi kamwe kufanya mazungumzo naye. Wote tunatambua wazi vishawishi ni kitu gani
, kwasababu wote tunashawishika, kwa mfano kuna vishawishi vingi kama vile kujipendekeza
,ubatili, kiburi, ulafi, uchoyo na vingine vingi Baba Mtakatifu anasema.
Leo hii watu wengi wanaongea suala la rushwa , hata kwa hilo tunapaswa kuomba msaada
kwa Mungu,kwasababu kuna rushwa nyingi Baba Mtakatifu anabaninisha na kusema,kuna
samaki wakubwa ambao wako duniani, ambao tunawasikia katika magazeti.Anatoa mfano
ya kwamba ,labda walianza nao kidogo kidogo , sijuhi labda wakati wa kupima kwenye
mzani, badala ya kufanya kilo moja wanaanza gram 900, ambayo inafanana na kilo moja.Rushwa
huanza kidogokidogo kama vile mazungumzo ya shetani , akisema “siyo kwamba tunda litakuharibu
, kula ni tamu!;kwa taratibu wakaanguka katika dhambi.
Kanisa linatufundusha tusiwe wepesi , usije ukasema ujinga, na hivyo Baba Mtakatifu
anasema li lazima kuwa macho na kuomba kwa Bwana kwasababu peke yetu hatuwezi.Adamu
na Eva walijificha kwa Bwana , lakini kinyume na sisi, tunahitaji neema ya Yesu ili
kurudi na kuomba msamaha.Baba Mtakatifu anarudia kusisitiza tena ya kwamba katika
vishawishi ni taadhali sana kufanya mazungumzo na shetani ,badala yake ni kuomba ukisema
nisaidie Bwana , mimi nimdhaifu.Sitaki kujificha , na hiyo ndiyo ujasiri wa kushinda.Kwani
ukianza mazungumzo utaishia kushindwa . Kwa njia hiyo Bwana aweze kutupa neema ya
katika safari kwa ujasiri ili tusipate kudanganywa katika udhaifu wetu na katika vishawishi.
Atupatie ujasiri wa kuamka na kuendelea na safari mbele, na ndiyo maana Yesu alikuja
kwaajili hiyo.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |