2017-02-09 16:15:00

Papa anasema mwanamke analeta maelewano ili dunia iweze kuwa nzuri



Bila mwanamke hakuna maelewano mazuri katika dunia, Mwanaume na mwanamke hawafanani lakini siyo kwamba mmoja ni bora zaidi ya mwingine , japokuwa siyo mwanaume bali ni mwanamke anayeleta maelawano ili dunia iweze kuwa nzuri.Ni maneno ya takakari ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa misa ya Alhamisi 9 Februari 2017 katika Kikanisa cha Mtakatifu Nartha Mjini Vatican, kwa kuelezea sura ya mwanamke tangia kazi ya uumbaji katika somo la siku kutoka kitabu cha mwanzo.
Baba Mtakatifu Francisko anaendelea na takafari lake juu ya kazi ya uumbaji na kusema Bwana alikuwa ameumba tayari wanyama , lakini mwanaume hakuwa na mwenza,alikuwa peke yake.Katika ubavu wa mwanamme Mungu akamtolea mwanamke .Mwanaume akamtambua mwanamke kama nyama yake, lakini Baba Mtakatifu  anaongeza akasema,kabla ya kumuona mwanamke kwanza aliota ndoto ,na hivyo ili kumtambua mwanamke ni lazima umuote.


Mara nyingi tunapoongea na wanawake , mara nyingi ujitokeza masuala ya kazi, ndiyo mwanamke ni kwaajili ya kufanya hivyo, pamoja na hayo anabainisha ya kwamba mwanamke anampelekea mali mwanaume ambaye hana mali kwa namna hiyo mwanamke anapeleka maelewano ya uumbaji. Kama hakuna mwanamke, hakuna hata  maelewano ,Baba Mtakatifu anatoa mfano wa watu, kwamba mara nyingi utasikia wakisema, hii ni jamii yenye tabia dume, maana yake anakosekana mwanamke.  Lakini mwanamke siyo kwaajili ya kuosha vyomba au kwaajili ya kufanya, bali mwanamke ni kwaajili ya kuleta maelewano . Bila mwanamke hakuna maelewano.Hawa wote siyo sawa na pia siyo kwamba mmoja ni bora zaidi ya mwingine, Baba Mtakatifu anakataa na kwamba mwanaume haleti maelewano , bali ni mwanamke anayeleta maelewano ambayo hufundisha hubembeleza , hupenda kwa moyo na ambaye ufanya ulimwengu uwe mzuri.


Baba Mtakatifu anachambua tafakari hili pia kwa namna tatu,ya kwanza ikiwa upweke wa mwanaume, ya pili ndoto na ya tatu mwisho wawote wawili yaani , kuwa mwili mmoja.Anatoa mfano dhahili kuhusu yeye, kwamba siku moja wakati wa akisalimiana na watu walio kuwa wamekuja Vatican,aliuliza wanandoa walio kuwa wakiadhimisha miaka 60 ya ndoa, ya kwamba ni nani kati yao alikuwa na uvumilivu?
Wao walimtazama kwa macho yao, na baadaye waligeukiana na kutazamana machoni,kitendo hicho Baba Mtakatifu Francisko anasaema hatakisahau kamwe, kwani baadaye walirudia kumtazama na kumjibu, kwamba sisi wote wawili,na tunapendana! Hiyo ndiyo kazi ya mwanamke anafanya ya kuwa na uwezo wa kupenda,pia maelewano na dunia.


Mara nyingi tunasikia ya kwamba siyo lazima katika jamii hii au katika taasisi uwepo wa mwanamke ambaye afanye hili wala lile hapana, utendaji si madhumuni ya mwanamke .Ni kweli kwamba mwanamke lazima afanya mambo, na nafanya kama sisi sote tufanyavyo .  Madhumuni ya mwanamke ni kufanya maelewano ,na bila mwanamke hakuna maelewano katika dunia. Kuwatumikisha watu ni uhalifu dhidi ya binadamu,lakini ni zaidi ya uhalifu wa kuharibu maelewano ambayo Mungu alipenda kutoa katika ulimwengu.

 
Mungu aliumba mwanamke ili wote tuweza kuwa na mama na kwa hiyo Baba Mtakatifu anamalizia akisema  mwanamke ni zawadi kubwa kutoka kwa Mungu,na katika Injili ya siku imesikia uwezo wa mwanamke jasiri , ambaye alikwenda mbele ya Yesu na kuomba amponye mtoto wake, kwa namna hiyo ni mwanamke mwenye maelewano ni utenzi na ni uzuri. Bila kuwa na mwanake katika ulimwengu hii dunia isingekuwa nzuri na isingekuwa na maelewano.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.