2017-02-09 17:30:00

Ndani ya mashua ya Petro, Civilta' Cattolica wapiga makasia


Ninayo furaha ya kukutana na nyinyi mkiwa na Jumuiya wa Jesuiti na watawa ambao wanashirikiana pamoja na nyinyi katika maisha ya  kazi ya magazeti na uendeshaji wa shughuli za nyumba mnazoishi .Ninapenda kutoa salam hata kwa wachapishaji ambapo wakati gazeti lenu litachapa kwa lugha ya kihispania , kingreza , kifaransa na kikorea.Nahisi pia uwepo wa familia nzima ya wasomaji wa magazetu yenu.Mmeunganika pamoja kwaajili ya kutangaza ripoti ya uchapishaji wa idadi ya  makala 4000.Ni hatua mojawapo ya kipekee ambayo gazeti lenu limepiga hatua ya safari  kwa kipindi cha miaka 167 na bado inaendelea kwa ujasiri kupiga makasia  ndani ya bahari iliyowazi.


Ni maneno ya baba Mtakatifu Francisko wakati wa kutoa hotuba yake kwa Jumuiya ya waandishi wa  Gazeti la Civilta Cattolica Alhamisi 9 Februari 2017 Mjini vatican .Baba Mtakatifu anasema ,na  tazama mbaki katika bahari ya wazi, Wakatoliki hampaswi kuwa na hofu katika bahari ya wazi, na wala kutafuta bandari ya hifadhi na usalama.Na hasa zaidi ninyi kama Jesuiti , jaribuni kukwepa na kutafuta sehemu zenye hifadhi na uhakika wa salama . Bwana anatutaka kwenda nje kufanya umisionari , kwenda mbali na siyo kustaafu na kulinda uhakika.Wakati wa safari ya mbali ndipo unakumbana na dhoruba na pia yawezakana  mawimbi tofauti, hata hivyo safari takatifu daima unakuwa na msindikizaji ambaye ni Yesu kwani mwenyewe anasema usiwe na hofu tazama ni mimi (Mt 14,27).


Baba Mtakatifu anasema,hampigi mbizi peke yenu, watanguli wenzangu,kama mwenye heri Papa Pio IX , Benedikto wa XV alipokutana nanyi wamewaunga mkono na kutambua mara nyingi kupiga mbizi kwenu katika mtumbwi wa Petro. Uhusiano huo kati ya mapapa daima imekuwa kipengele muhumu cha gazeti lenu.Nyinyi mko ndani ya mtumbwa wa Mtakatifu Petro na mara nyingi katika historia kama ya jana , siyo cha kustaajabisha ya kwamba mawimbi yanaweza kuchafuka .Lakini hata mabaharia waliokuwa mstari wa mbele ndani ya mashua ya Petro walipiga makasia kuelekea nyuma.Daima jambo hilo limejitokeza. Nyinyi kama Gazeti la Civilta' Cattolica mnapaswa kuwa wazoefu wa wapiga makasia mashuhuri na wenye thamani.

 

Toleo la makala 4,000 siyo mkusanyiko wa makaratasi tu  bali ndani yake kuna maisha yenye kuwa na tafakari nyingi,yenye kuwa na shahuku nyingi sana , mapambano endelevu na utata ulio jitokeza, lakini zaidi ya yote kazi nyingi.Baba Mtakatifu anasema ya kwamba anajua ya kwamba Mababu zao wa zamani walipendelea kuitwa wafanyakazi , na siyo wasomi, bali wafanyakazi. Ninapenda sana ufafanuzi huu kuonesha unyenyekevu, uzuri na upole.Mtakatifu  Ignatius anataka wafanyakazi kama wafanyavyo kwenye shamba la mizabibu kwa maana ya kila mmoja nafanya kazi karibu na mwenzake.Na wote tuko pamoja, mimi katika kazi yangu lakini ninawaona , ninawafuatilia , na kuwasindika kwa upendo. 

 

Gazeti lenu mara nyingi Baba Mtakatifu anasema lipo mezani kwangu, kwa njia hiyo kazi yenu haipiti kamwe machoni pangu. Anawapa pongezi ya kwamba mmefuatilia kwa uamininifu hatua zote za kuchaguliwa tangu mahojihano marefu ambayo nilikubali kutoa kwa mkurugenzi wenu mwaka 2013,kutangazwa kwa Ensiklika na  hati za kitume , kwa kutoa ufafanuzi wa uaminifu , sinodi, ziara za kitume , na jubileo ya huruma, kwa hayo yote ninawashukuru  na kuwaomba muendelee na njia hiyo ya kufanya kazi na mimi na pia kusali kwaajili yangu.

 

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.