2017-02-08 16:02:00

Ni watu maskini na waliotengwa mara nyingi hufundisha kutumaini


Ndugu tunawahimiza muwaonye ndugu walio na wavivu , mwatie moyo watu wanyonge , muwasaidie watu wadhaifu, muwe na subira kwa wote.Angalieni mtu yeyote asimlipe mwingine maovu kwa maovu , ila nia yenu iwe kutendeana mema daima na kuwatendea mema watu wote.Furahini daima , salini kila wakati  nakuwa na shukrani katika kila jambo, hayo ndiyo anayotaka Mungu kwenu katika kuungana kwenu na Kristo Yesu." Jumatano iliyopita tulimwona Mtakatifu Paulo katika somo kutoka  barua ya kwanza ya Watesalonike akishauri tubaki kidete katika matumaini ya ufufuko,wakati huo huo Mtakatifu anatuonesha kwamba matumaini ya mkristo siyo pumzi binafsi , bali ni ya kijumuiya na kikanisa..Ni manaeno ya utangulizi wa katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 8 Februari 2017 katika ukumbi wa Paulo wa VI , Baba Mtakatifu anendeleza katekesi katika mfululizo wa matumaini ya Kikristo!

Kwa mtazamo huo Mtakatifu Paulo anajikitia katika uwanja mkubwa zaidi kwa hali halisi inayounda jumuiya ya kikristo, akiwaomba wao wasali kwa ajili ya wengine na kusaidiana wao kwa wao.Hiyo siyo kwa bahati mbaya yeye kuwafanya wao ambao amewakabadhi kuwajibika na kuongoza utume.Hiyo ni kwasababu Baba Mtakatifu anasema,ni wao wa kwanza wanao paswa kukuza matumaini, na siyo kwasababu wao ni bora zaidi  ya wengine bali ni kwa nguvu za utume wa Mungu ambao unakwenda juu zaidi ya mategemeo yao.Kwa sababu hiyo hawana budi kuwa na heshima , kuchukuliana wao kwa wao na kuwa wakarimu kwa wote.

Mtazamo zaidi wa somo hilo  unajikita hasa kwa wale ndugu ambao wanakaribia kuathrika katika kupoteza matumaini, na kuangukia kwenye mahangaiko.Na kwa njia hiyo inawalenga walio poteza ujasiri, ni wadhaifu na wanajisikia kuelemewa  na mizigo ya maisha na dhambi zao ,na kushindwa kutatua matatizo yao. Katika hali hii ni jumuiya yote ya Kanisa inayo paswa kuwajibika kuwa karibu nao na kwa kina kuonesha upendo wa dhati , na wanapaswa kuwajibika kuonesha mara nyingine uhuruma, kuwajali na kuwatuliza. Hiyo ndiyo njia muhimu kwasababu matumaini ya mkristo hayawezi kamwe kutokufanya tendo la upendo wa dhati.


Hata Mtume wa mataifa mwenyewe katika barua yake kwa Waroma anasema kwa moyo wote ya kwamba “Sisi tulio imara katika imani tunapaswa kuwasaidia wale walio dhaifu wayakabili matatizo yao. Tusijipendelee sisi wenyewe tu. (War 15,1). Baba Mtakatifu Francisko, anasema ushuhuda huu kama wakristo haupaswi kubaki ndani ya ngome umefungwa katika jumuiya bali unapaswa usikike sauti yake  hata nje ya kwa  mantiki ya jamii na raia. Baba Mtakatifu anasisitiza akisema Kama wito , msitengeneze ngome bali ni madaraja , na msijibizane mabaya kwa mabaya , bali kushnda ubaya kwa wema , msikasirishane, bali kusamehe, na kuishi kwa amani na watu wote. Baba Mtakatifu anasema na hiyo ndiyo maana ya Kanisa, na ndiyo matendo ya matumaini ya kikristo , anapokubali kwa nguvu na wakati huo huo kushikiria upendo wa ukarimu.

Kwa njia hiyo inaonesha wazi ya kwamba hutuwezi kujifuza  kutumai peke yetu. Ili kukuza na kulisha matumaini , tunalazimika kuwa na kikundi kama mwili wa kusaidiana kwa pamoja ili kuweza kuishi. Kwa namna hiyo iwapo mimi ninatumaini, maana yake wamekuwapo watu walio saidia kunifundisha kutumaini, na kuweka hai matumani yetu.Miongoni mwa hao, Baba Mtakatifu anasema naweza kuwanyambulisha kama vile walio wadogo yaani masikini, watu rahisi wasio kuwa na haki na walio tengwa.Anaye jifungia binafsi katika utajiri wake , na mali zake na kujisikia kila kitu ni sawa katika maisha yake , hakika  hawezi kamwe kutambua matumaini.Badala yake wanao tumaini, ni wale ambao kila siku wanapata majaribu, udhaifu na vikwanzo vyao.  Ndiyo hawa ndugu zetu wanao tupatia ushuhuda mzuri na wenye nguvu,kwasababu hubaki imara katika kujikabidhi kwa Bwana , wakitambua kwamba zaidi ya kwamba huzuni , uonevu na kukabiliwa na kifo siyo neno la mwisho bali neno la mwisho litakuwa ni huruma uzima na amani.

Baba Mtakatifu anamalizaia akisema kwamba , asili na makao  ya matumaini  ni mwili wa  mshikamao , kwa upande wa matumaini ya kikristo, mwili huo ni Kanisa , wakati huo pumzi ya maisha ni matumaini ya Roho Mtakatifu.Ndiyo maana Mtakatifu Paulo anatualika mwisho akitamka bila kuchoka, na hasa tusipotaka kuanguka, tunapaswa kutumaini.Lakini roho mtakatifu akiishi ndani mwetu , yeye utufanya tutambue ya kwamba tusiogope , maana Bwana yu karibu na anachukua jukumu kwaajili yetu , ni yeye anaye panga jumuiya zetu , kwa njia ya Pentekoste kama ishara inayo onekana ya matumaini kwa familia nzima.

Mara baada ya katekesi yake, Baba Mtakatifu  kama kawaida yake ya salam kwa wote , kwa namna ya pekee aliwasalimu wanakamati yasiku ya dunia ya kupinga na kukomesha biashara ya watumwa , vijana , waliodhuria mkutano wa Chama cha vijana wa Ulaya , na mahujaji wengi waliofika,bila kuwasahau vijana wengine, wagonjwa na wana ndoa wapya.Alikumbuka ya kwamba tarehe nane ya kila mwaka ni siku ya kukumbuka Mtakatifu Bhakita,sanjari na siku ya kupinga biashara ya binadamu Duniani na hivyo anasema Mtakatifu Bakhita  alifanya uzoefu wa kuathirika na bishara ya utumwa. Kwa njia mfano wa utakatifu , vijana waweze kuwa na  mwamko wa kuwasaidia vijana wenzao walio wadogo na wenye matatizo.Na kwa wagonjwa anawaeleza , watoe mateso yao kwaajili ya elimu ya kikristo kwa kizazi kipya. Na mwisho wana ndoa anawatia moyo wana ndoa wapya katika kujikabidhi kwa Mungu na siyo kwaajili ya uwezo wao binafsi.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.