Tangu tarehe 28 Januari hadi yarehe 3 Februari 2017, Askofu Mkuu Paul R. Gallagher
, Katibu wa Mahusiano ya nchi za Nje wa Vatican , alifanya ziara maalum huko Japan
kwa mwalimko wa viongozi .
Askofu mkuu akiwasili huko 28 akiwa amesindikizwa na Monsinyo Roberto Lucchini , mshauri
wa Balozi katika ofisi ya Katibu wa nchi na kupokelewa uwanja wa ndege wa Narita na
Askofu mkuu Joseph Chennot , Balozi wa papa wa kitume huko Japan na Balozi wa Vatican
Askofu Yoshio Matthew Nakamura , na Katibu wa Balozi wa Papa huko Japan Mons. Paweł
Obiedziński na wawakilishi wa Baraza la maaskofu wa Japan.
Siku aliyofika alipata kukutana na wawakilishi wa Kidplomasia wa serikali ya nchi
akiwemo Waziri wa Uchumi ,Nobuteru Ishihara,ambapo Katibu wa mahusiano na nchi za
nje Askofu Mkuu Gallagher alielezea juu ya mshikamano na ushirikiano ambao ulianzishwa
na mahusiano ya kale ya utamaduni na kiroho , na kwamba leo hii umepata kujieleza
thabiti katika ahadi ya kueneza amani na pia kwaajili ya upungufu wa silaha za kinyukilia
, na kwa kushirikiana na nchi zinazoendelea na kulinda mazingira.
Tarehe 29 Januari baada ya misa katika kanisa Kuu la Tokyo Askofu Mkuu Gallagher alikwenda
Hiroshima , na tarehe 30 Januari katika omelia yake katika misa ya haki na mani iliyoadhimishwa
katka Kanisa kuu la kumbukumbu , alipenda kumbuka historia ya ziara ya matembezi ya
Mtakatifu Yohane Paul wa Pili aliyetamka kwamba amekwenda kama muhujaji.
Baada ya misa ya tarehe 31 Januri katika Shirika la wasalesiani Akabane kando ya mji
wa Tokyo, Askofu Mkuu alikutana na Waziri mkuu Shinzo Abe.Wakati wa mazungumzo yao
walionesha ushirikiano mzuri kwa ngazi ya nchi zote mbili na haja ya kutahidi kuwa
pamoja katika maendeleo dhabiti na ya amani katika nchi. Hali kadhalika Waziri Mkuu
alikumbuka kwa shukrani kupokelewa na Baba Mtakatifu Francisko mnamo mwaka 2014 ,
ambapo alitaka kwa namna ya pekee amfikishie mwaliko wa maombi ya ziara yake kwa
niaba ya watu wa Japan.
All the contents on this site are copyrighted ©. |