2017-02-04 15:10:00

5-8 Mei 2017 mwaliko wa kirafiki kati ya wakristo na waislam


Tarehe 5 hadi 8 Mei 2017, Jumuiya ya kiekumene ya Taze huko Ufaransa itapata ugeni kufanya urafiki ambao unataka kuwaunganisha wakristo na waislam.Walio andaa tukio hilo ni kikundi cha Waislam na wakristo  kwa ushirikiano wa ndugu wa Jumuiya ya kiekumene Taize.Taarifa inasema kwamba watu wote walio zoea kwenda kwenye kituo hicho kwa sala wanaalikwa katika urafiki huo na waislam,na wakisistiza hasa wafike kwa wingi vijana kuanzia miaka 18 hadi 35.


Kauli mbiu ya mkutano na urafiki huo ni “niamkapo nishibishwe kwa sura yako Mungu. Pamoja na shughuli ambazo wamezeoa kufanya, maandalizi ya mkutano wa sala una lengo kuu la kutambuana wao wa kwao kati ya wakristo na waislam.Vilevile taarifa inasema kwamba wakati wa sala,utandaliwa ukumbi mkubwa kwa waislam wote wapate kusali, halikadhalika wakristo wote watakwenda katika kusali kwenye Kanisa la mapatano la Jumuiya ya kiekumene.Ni mengi yatakayo jadailiwa lakini miongoni ni  pamoja na  uhuru wa kujieleza ,kazi ya walei, heshima ya mambo matakatifu, na hasa kwa upande wa vitabu ambavyo mara  nyingi taarifa inasema uleta utofauti  kati ya dini lakini siyo waamini wanaoshi katika jamii moja.

 

Watakao toa hotuba  ni pamoja mtunzi wa mashairi Khaled Rounmo, anayejikita  kwa juhudi zote juu ya mazungumzo ya utamaduni na dini, Ralph Stanely Mkufunzi wa Teolojia ya kiprotestanti katika Chuo Kikuu Strasbourg, Khaled Ben Tounès kiongozi wa kiroho wa Jumuiya ya sufi Alawiyya, vilevile ndugu Aloy Mkuu wa Jumuiya ya Taize . Kahina Bahloul, Rais wa chama cha Kiislam , Mirelle Akouala mchungaji wa Kanisa la Kiprotestanti  wa Ufaransa . Watazungumza kwa kina juu ya mada ya sala kuhusu kuhabarisha wakiongozwa na sehemu mbili za masomo kutoka katika Korani na Biblia sehemu ya Kupshwa habari Maria ambayo inapatikana sehemu zote mbili za Koran na Biblia.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.