Katika Jumuiya za wahamiaji wanaoishi nchini italia wapo wanawake wengi waathirika
wa uketaji na asilimia kubwa inatofautiana kulingana na asili ya nchi yao. Makadirio
ya mwaka 2016 inaonesha idadi ya wanawake wageni ,wamekeketwa ambapo ni wanawake kati
ya 46,000 na 47,000 hizo ni takwimu zilizotokana na wanaweke vijana walio jifungua
watoto nchini Italia. Na zaidi ya asilimia 60 ya wanawake walio nchini Italia wameonesha
kutoka nchi ya Nigeria na Misri.
Lakini Ukifikiria kiwango cha waathirika kwa ujumla ni wanawake kutoka nchini Somalia
walio athirika zaidi ya kwasababu ni asilimia 83,5% wakifuatiwa wanaotoka Nigeria
asilimia 79,4% na Burkina Faso asilimia 71%.Halikadhalika jamii ya Misri (60.6%),
Eritrea (52.1%), Senegal (31%) na Ivory Coast (11%).
Hayo ni baadhi matokeo ya utafiti uliofanywa na mradi wa Daphne MGF –PREV unaoendeshwa
nchini Italia katika Chuo Kikuu cha Bicocca Milano kwa lengo la kikadiri ukubwa wa
hali halisi ya watu walio pata uzoefu wa kuathirika na ukeketaji huo miongoni mwa
jamii inayoishi katika nchi ya Italia.Matokeo hayo yaliwasilishwa tarehe 1 Februari
2017 kwenye Chuo Kikuu Bicocca Milano katika Mkutano ulio andaliwa na Shirika la
ActionAid na chama cha Utamaduni katika mtazamo wa Siku ya Kimataifa ya kupinga ukeketaji
wa wanawake, itakayo fikia kilele chake tarehe 6 Februari 2017.
All the contents on this site are copyrighted ©. |