2017-01-31 15:49:00

Kwa kufuata sheria na usalama wakimbizi 40 waingia nchini Italia


Wakimbizi 40 zaidi kutoka Syria , kati yao wakiwemo watoto na wanawake , waliwasili katika uwanja wa kimataifa Fiumicino nchini Italia tarehe 30 Januari 2017, hiyo ni kutokana na mpango wa  njia za kibadamu za Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, Shirikisho la Makanisa ya Kikristo ya Italia na Kanisa la Kibaldesi. Mpango huo ulianza 2015 ambao umewazesha watu 500 kufika Ulaya kwa ruhusa halali.Ni mfano unatoa huduma harambee kati ya mashirika ya kiraia na Wizara ya Mambo ya nje na ya ndani ya Italia.Mpango huo unatarajiwa kufika watu 1,000 kufikia mwisho wa mwaka 2017.
Mhusika wa sekta ya Wahamiaji katika Jumuiya ya Mtakatifu Egidio Daniela Pompei anaeleza zaidi juu ya  makubaliano ya watu wapya waliofika, akihojiana na mwandishi wa Habari wa Radio Vatican ya kwamba watu waliofika ni familia wakiwema mama , baba na watoto, lakini pia wakiwemo wazee , yaani watu wazima wapo pia wasio kuwa na familia, ikiwa ni pamoja na wawili waliotoka gerezani.Na kwamba wageni hawa wote watakuwa wenyeji kwenye mikoa mingi ya Italia.


Hawa wote na wengine watakaofika watagawanywa katika mikoa yote na wilaya amabayo ni ishara ya makaribisho makubwa , kwani ni jumuiya mbalimbali za Parokia na ndani ya familia watakao wapa makaribisho. Anaongeza Daniela kuwa mfano huo kukaribisha umeanza kufanyiwa majaribio ya kanda hizi za kibinadamu ambayo pia inajihusisha katika kuhakikisha wageni wana ungana na kuzoea  jamii.
Hali kadhalika kuhusu mpango huo ulioanza 15 Desemba 2015 baada ya mkataba wa kiekumene  kutia sahini na Waziri wa Mambo ya Nje na ya Ndani ya Italia anaeleza kwamba baada ya mkataba huo , familia za kwanza walifika tarehe 4 Februari 2016 na wengine wengine  wakafika tarehe 29 Februari 2016, hadi kufikia leo hii ni, watu 540 wameshawasili kwa  ndege tofauti  mara sita. Licha ya hayo pia wanatazamia kufikia mwisho wa mwezi Februari 2017 watu 120  watawasili , na wote karibia ni kutoka nchi ya Syria, japokuwa yupo mmoja kutoka Iraq kwasababu walikutana naye nchini Lebanon.


Daniela anasema uzoefu huo ni chanya na mzuri kiasi cha kusifiwa na ngazi ya kimataifa kusema kwamba ni mfano wa kuigwa.Pamoja na hayo anaongeza kwamba hata  Baraza la maaskofu wa Italia wame andika protokoli ya kuongeza watu wengine 500 , kwa namna hiyo njia sasa italenga kuwapokea watu kutoka upande wa Afrika. Protokoli ambayo imesha andikwa, anasisitiza,  inatazamiwa watu 1,000 ambapo watu 540 wameongezwa, kwa namna hiyo kufika mwisho wa mwaka 2017 watu wote hao watakuwa wamepokelewa,na wakati huo huo protokoli inayotazamiwa watu wengine 500 watafika kutoka nchi ya Ethiopia, Eritrea , Kusini mwa Sudan na Somalia.

 
Mfano huo ni wa kibinadamu kwa unao jikita katika  usalama na sheria , kwa njia hiyo anasema Daniela wao wanataka waeleze  ulimwengu ya kwamba upo uwezekano mwingine wa kufanya watu waingie , na siyo waingia kupitia mikono ya watu waalifu, njia hiyo siyo ya Bahari na kusababisha vifo majini.Kuna uwezekano mwingine ambao nchi zinaweza kuutumia ambapo nchi ya Ufaransa inakaribia kuandika protokoli, iliyo tangazwa na Waziri Mkuu Cazeneuve ambao unatazania  kuwashirikisha makanisa ya kiinjili ya Ufaransa na Jumuiya za Mtakatifu Egidio , na Baraza la maaskofu wa Ufaransa: Ni matumani yao kwamba hata Ulaya wanaweza kuiga mfano huo kwasababu ni mfano thabiti unatoa usalama kwa wakimbizi na zaidi kulinda usalama hata kwa ajili ya wazalendo wa Ulaya.

 

Sr Angela Rewezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.