2017-01-30 15:35:00

Uganda: Mgonjwa wa kwanza kupona kwa ugonjwa sugu wa kifua kikuu


Kituo cha afya cha Lorengachora huko Uganda wamefanya sherehe kutokana na kupona kwa mgonjwa wa kwanza aliyekuwa amepatwa na ugonjwa sugu wa kifua kikuu baada ya miaka miwili ya tiba. Hiyo ni moja wa matokea ya ufanisi walio uleta ndani ya nchi  Madaktari na Afrika CUAM.
Taarifa kutoka Shirika la habari la Fides linasema ,tangu mwaka 2014 Madaktari na Afrika walianza kazi hiyo ya kutokomeza ugonjwa sugu wa kifua kikuu katika ukanda wa Karamoja wakisaidiwa na msaada wa Kimataifa wa Huduma (FAI), pamoja na kikundi cha madakatari kutoka Hosptali ya Metany Milano Italia.

Ugonjwa sugu wa kifua kikuu ni ugonjwa unao enea kwa urahisi na hasa katika mazingira ya msongamano, pamoja na hayo yote suala la kutibu ugonjwa huo ni mgumu na hukuchua muda mrefu.Kwa mujibu wa Cuam hadi sasa wagonjwa walio tambuliwa katika ukanda huo ni ni 13, wanatibiwa manyumbani mwao , lakini wakiwa wanarejea mara kwa mara katika kituo cha afya kwa matibabu.
Shirika linajihusisha na hatua zote kwa wagonjwa kuanzia kutoa usafiri, kuchunguza upatikanaji wa dawa, kusimamia wafanyakazi wa ndani . Hata hivyo wanasema  mwanzo walikuwa wanajihusisha  na jukumu la kutoa huduma ya chakula kwa wagojwa wakati wa matibabu hasa wagonjwa ambao hawakuwa na uwezo, lakini serikali imekubali kuchukua jukumu la suala hilo.

 

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.