2017-01-30 14:58:00

Mons. Oliver kupongeza Kanisa Katoliki Zambia kwa ulinzi wa watoto


Tume ya Kipapa kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto wameipongeza Kanisa Katoliki Zambia kwa kuwalinda watoto na watu wazima wanao ishi katika mazingira magumu.Katibu Mkuu wa Tume ya  Kipapa kwa ajili ya ulinzi wa watoto Monsinyo Robert Oliver  anasema,Kanisa la Zambia linapaswa kupongezwa kwa kuzungumza kwa moyo wote na kuchukua hatua  katika kushughulikia suala la unyanyasaji wa watoto.


"Nilipokutana na Askofu Mkuu , aliongea kwa nguvu juu ya mahitaji na ya kuhakikisha kwamba kila mtoto ni salama na anakua katika mazingira ya Amani na upendo.Yapo mambo  yanayo tokea  hapa nchini Zambia ya kusisismua na kupengezwa" .Anasema Minsinyo Olver .
Halikadhali anatoa wito kwa jamii ya kutojihusisha na unyanyasaji wa kijinsia,pia  dhidi ya kufanya ngono kwa mtoto yoyote.
Anasema "Unyanyasaji wa kijinsia  kwa mtu ni mbaya. Hatupaswi kuficha wahalifu hawa; haijalishi kama ni mtu mwenye mamlaka katika Taasisi, mapadre katoliki, mjomba au Baba.Tunapaswa wote kwa pamoja kupinga viendo hivi.Kwa njia hiyo ni kazi yetu kupitia mashirika yote ya dini katoliki, vyama vya kiraia na wengine".


Monsignor Oliver aliyasema hayo  alipokuwa Zambia kama  mjumbe kwenye warsha ya siku moja huko mjini Lusaka, Jumatatu,23 Januari 2017. Kauli mbiu ya  warsha ilikuwa juu ya "haja ya kutekeleza Sera katoliki  juu ya ulinzi wa Watoto na wanaoishi katika mazingira hatarishi katika jamii" kama kama wito wa  Baba Mtakatifu Francisko , kwani amewataka Kanisa kufanya maamuzi ya kuwalinda watoto na vijana wa dunia nzima.

Kutoka Amecea Blog

 








All the contents on this site are copyrighted ©.