2017-01-29 13:40:00

Ukosefu wa uaminifu ndani ya jumuiya ni moja ya changamoto ya sasa


Uwepo wenu ni sababu ya furaha yangu kuwapokea wakati mmeunganika katika Mkutano Mkuu wa Mwaka kwa kutafakari juu ya Imani kwenye  kujikabidhi,na Hotuba yake aliyoitoa  Rais wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Taasisi za kitume  pia salam kwa wote nikiwaonesha kuitambua  kazi yenu katika huduma ya maisha ya kitawa kwa Kanisa.


Ni maneno ya utangulizi wa hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko alipokutana na washiriki wa Mkutano wa Mwaka kwa mashirika ya maisha ya Kitawa na vyama vya kitume Jumamosi 28 januari 2017 mjini Vatican. Anasema kauli mbiu mliyochagua ni muhimu , ambapo tunaweza kusema kwa nyakati hizi uaminifu ni changamoto ya majaribu, kutokana na takwimu mlizo onesha.Baba Mtakatifu anatoa mfano kwamba chanagamoto hiyo inafananishwa na damu zisizosimama, ambazo udhoofisha maisha ya kitawa na Kanisa yenyewe.Kitendo cha wengi kuacha utawa, kinaleta wasiwasi mkubwa.Ni kweli kwamba wengine wanaacha kutokana na sababu za msingi , kwasababu wametambua nafsini mwao mara baada ya safari yao  ya kiroho ua kwamba hawana wito, lakini licha ya hayo wapo  wengine ambao wanakosa uaminifu, anaongeza na kusema hayo yanajitokeza mara tu  baada ya kufunga nadhiri za milele ,Je ni kitu gani kimesababisha ? Ni swali Baba Mtakatifu anauliza.


Kama vile mlivyo onesha ya kwamba zipo  sababu zinazosababisha ukosefu wa uaminifu, kwa njia hiyo mabadiliko  ya mihongo na siyo tu mabadiliko ya mihongo , bali jinsi ya kuweza kukabiliana na utata na kuchukua majukumu thabiti ya kudumu.
Sababu ya kwanza inayofanya kutokutunza uaminifu ni mazingira ya kijamii na utamaduni  tunamoishi.Tunaishi katika utamaduni ulio gawanyika vipende vipande ,kwani kitendo cha kutaka kutunisha mfuko, unamfanya mtu aishi kwa mitindo . Huo ni utamaduni unaofanya mtu kuishi akitegemea milango mingine ya pembeni inayofungua uwezekano  mwingine. Kitendo cha kutegemea milango hiyo  inaongeza matumizi na kusahahulisha uzuri wa wa maisha rahisi na ya kina na kusabaisha utupu wa kuishi.

Baba Mataktifu anaelezza kwamba,imejitokeza sababu za vitendo vya mahusihano kulingana  na jinsi kila kitu ni kuhumu katika suala binafsi ,na mara nyingi ni tofauti na maadili ya Injili. Tunaishi katika jamii ambapo sheria za kiuchumi huchua nafasi ya kwanza zaidi ya maadili , Watunga sheria hulazimisha kwa manufaa yao mwenyewe , wakikandamizu thamani ya maadili ya maisha.Na hiyo ni jamii ambayo udikteta wa fedha na faida zake umwondolea yule ambaye hana uwezo , kwa mantiki hiyo ni wazi  kwamba mtu lazima kwanza ache kuhubiriwa ,na ajibidishe baadaye kuhubiri.
Katika sababu ya Utamaduni jamii, tunapaswa pia kuongeza  sababu nyingine. Mojawapo ni ulimwengu wa vijana , huo ni ulimwengu tata Baba Mtakatatifu anasema , wakati huo pia umejaa  changamoto. Lakini hapakosekani hata vijana wakarimu, wenye kuwa na mshikamano na wanao jibidisha katika ngazi ya mambo ya kidini na kijamii.Ni vijana wanaotafuta ukweli wa kiroho, vijana wenye njaa  ya jambo flani tofauti ili wapate kuipeleka  duniani.Baba Mtakatifu anasisitiza kwamba wapo ndiyo vijana wakarimu na siyo wachache. Pamoja na hayo, wapo miongoni mwa vijana waathirika katika  mantiki ya kiulimwengu , ambao wanatafuta sifa  , kwa njia zozote, au fedha rahisi na anasa.


Mantiki hii inawaada vijana wengi, na hivyo hughuli yetu kubwa , siyo tofauti  ya kukaa karibu nao  kwa kutoa ushuhuda wa Injili ya furaha itokayo kwa Kristo.Ni utamaduni unao paswa kuwahabarishwa iwapo hatutaki vijana wasitafunwe na ulimwengu huu.
Sababu ya tatu ni ile inayotoka ndani ya maisha yenyewe ya utawa ,kwani mbele ya ukaribu wa utakatifu Baba Mtakatifu anasema hapakosi hali ya kutokuonesha ushuhuda , ambayo hufanya uaminifu kuwa mgumu. Kati ya hali hizo ni sababu hizo za ndani ya jumuiya ni pamoja ukawaida, uchovu,madaraka ya usimamizi wa nyumba, mgawanyiko wa ndani, kutafuta ukuu,shirika kutawaliwa na mitindo ya kiulimwengu, au namna ya kutawala kibavu wakati mwingine husababisha mazoea ya kufanya hali ya maisha yaende hivyo.


Baba Mtakatifu Francisko anatumia maneno ya Mtakatifu Paulo ya kwamba iwapo maisha ya utawa yanapaswa kubaki katika utume wake , yanapaswa kubaki katika msimamo wake , na kuendelea kuwa katika shule ya uaminifu kwa walio karibu na mbali.(Ef 2,17),Inapaswa kutunza upya wake na habari mpya ya kiini cha Kristo kwa njia ya roho na nguvu ya kitume , kuonesha uzuri wa kumfuasa Yesu na kuangaza kwa matumaini na furaha.
Moja ya eneo lionapaswa kutilia umakini wa kutunza katika kutunza  maisha ya kindungu ndani ya jumuia.Ni lazima kulishwa kwa sala , kusoma Neno, kushiriki kikamilifu katika sakramenti ya ekaristi , ya maridhiano na mazungumzo ya kindugu , na kuwa na mawasiliano ya dhati kati ya wanajumuiya wake, aidha kusahihishana kindugu, kuanzia huruma  kuelekea kwa ndugu aliye kosa , na kwa kushirikishana majukumu.


Yote hayo yafanyike kwa furaha na ushuhuda wa maisha rahisi , hasa kujitoa kwa masikini wanaoishi pembezoni.Vilevile kufanywa upya katika maisha ya kidugu ndani ya jumuia , inategema sana na utume wa miito , usema njoo na uone ( Jh 1,39) na kuishi kwa pamoja kindugu wawe vijana au  wazee .Na hiyo ni kwasababu  kama kijana hapati mahitaji muhimu katika maisha ya kitawa ndani ya jumuiya atakwenda nje kutafuta .( Soma Ujumbe wa  maisha ya Jumuiya ya watawa wa Tarehe 2 Februari 1994, 32).

Wito ni kama vile imani hiyo ni tunu ambayo tunaichukua kwenye  mtungi wa mfinyanzi (2 Kor 4,7) kwa namna hiyo  tunapaswa kuitunza kama watunzavyo vito vya thamani, ili baadaye isije ibiwa hiyo tunu hiyo na wala kupoteza uziri wake baada ya kupita muda .

 

Wajibu huo hawali ya yote ni kwa kila mtu ambaye ameitwa kumfuata Yesu Kristo kwa karibu kwa imani , matumaini na Upendo. Hivyo Baba Mtakatifu ana waalika kujihimarisha kila siku katika sala na kuweka nguvu  kwenye mafunzo ya kiteolojia na mafunzo ya  kiroho, ambayo inapinga na kuzuia mitindo ya utamaduni wa kisasa ili kuweza kutembea kidete katika imani.
Kwa misingi hiyo ni wazi kwamba upo uwezekano wa kufuata mashauri ya kiinjili na kufanana na mawazo ya Kristo(Fil 2,5). Wito ni zawadi ambayo tumeipokea kutoka kwa Bwana,inayojikita upendo wake kwetu sisi alivyo tupenda (Mk10,21) na kutuita tumfuate  katika maisha ya kitawa,wakati huo unawajibisha kila mto aliyepoka zawadi hiyo.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.