2017-01-28 10:34:00

Papa:Wakatoliki na Waorthodox sote tumebatizwa kwa Roho mmoja


Natazama kwa furaha kubwa kazi ya Kamati yenu iliyoanzishwa tangu 2003 ambayo imefikia mwaka wa 14 wa kamati hiyo. Mwaka jana mlitafakari kwa kina juu ya mwanzo wa Sakramenti , kwa namna ya pekee juu ya Ubatizo. Kwa hakika ni katika ubatizo ambapo sote  tumegundua msingi ya umoja wa kikristo , wakatoliki na waotodosi wa mashariki tunaweza kurudia  kusema  kama vile Mtume  Paulo kwamba “sisi sote tumebatizwa  kwa roho mmoja “ na sisi ni mwili mmoja (1Kor 12,13). Kwa wiki hii mmejikita  sana katika kutafakari  mantiki za kihistoria , kiteolojia , kikanisa na ekaristi takatifu,ambayo ni chemichemi ya maisha ya kikrsto, inayo jitambulisha katika kukamilisha umoja wa watu wa Mungu (Mtaguso wa VAT. II, Mwanga wa mataifa Lumen gentium,11).Kwa kuwatia moyo , ninayo matumaini ya kwamba kazi yenu inaweza kwaelekeza misingi muhimu katika safari ili  kusaidia mwendo hadi kufikia siku inayo tamaniwa ambapo tutakuwa na neema ya kuadhimisha sadaka ya Bwana mbele ya Altare , kama ishara ya umoja wa Kanisa uliojaa na thabiti.

Ni sehemu ya hotuba ya Baba Mtakatifu aliyoitoa Ijumaa 27 Januari 2017 kwa Wanakamati wa Kimataifa kwa ajili ya Majadiliano ya kitaalimungu kati ya Kanisa Katoliki na  Makanisa ya Kiotodosi ya mashariki. Baba Mtakatifu anasema, wengi wenu mantoka katika nchi ambazo kila siku kuna mshambulizi ya kigaidi na vitendo vya kutisha, tuna utambuzi wa hali ya mateso makubwa , yanayozidi kutanda mizizi na hasa kwa watu walio masikini,wasio kuwa na haki, wakubaguliwa na jamii, ambayo imesababishwa na ubinafsi .Ni lazima kutafuta njia ya kutatua migogogoro ambayo imezidi kuzaliana na kusabisha vita na umasikini na chuki. Lakini Baba Mtakatifu anasema kila siku makanisa yenu yako karibu na wote wanao  teseka ,mkiwaalika wapande mbegu ya maelewano na kujenga subira  ya matumaini, kuhamasisha amani itokayo kwa Bwana, ambayo ndiyo wito wetu katika dunia.

Mtakatifu Paulo anaandika  “Kiungo kimoja kikiumia , viungo vyote vya mwili pia”  (1 Kor 12,26).Mateso hayo, ni sawa na mateso yetu . Ninaungana  nanyi  katika sala , uwep mwisho wa vurugu , na pia niko karibu na watu wote walio athirika na zaidi watoto, wagonjwa na wazee.Vile vile niko karibu kwa moyo wote na maaskofu, mapadre, watawa, waamini na waathirika waliotekwa nyara na kulazimshwa kuwa watumwa.Halikadhalika  Papa anasema , watakatifu wanaweza kuwa nguzo  ya wakristo kwa ajili ya maombi kwani wao ni mfano wa wafia dini na watakatifu jasiri  na kutoa ushuhuda kwa Kristo.Wao ni mfano wa kuigwa kwa moyo wao wa imani, na siy tu kuonesha kwa ujumla ujumbe wa amani na maridhiano , bali Yesu mwenywe , msulibiwa na aliyefufuka , yeye ni amani yetu na maridhiano ( Ef 2,14; 2 Kor 5,18).Kama mitume wake tunaitwa kutoa ushuhuda kila sehemu kwa nguvu ya ukristo,  upendo wa kinyenyekevu ambao utoa mapatano ya binadamu wa kila nyakati.

Pale ambao kuna vita uzaa vita  na pia kifo , Injili ni jibu na chachu amabayo ufanya kuzaa matunda ya maisha hata katika jangwa hutoa majani ya matumaini baada ya usiku wa kiza na hofu.Kiini cha maisha ya Kikristo ni fumbo la Yesu kufa na kufufaka kwa ajili ya upendo , ndiyo msingi mkuu wa safari yetu  kuelekea umoja. Mashahidi  kwa mara nyingin tena , wanaonesha njia.Ni mara ngapi wakristo wamejitoa sadaka vinginevyo ni kugawanyika juu ya mambo mengi ya kuwa na umoja. Wafia dini na watakatifu wa tamaduni zote za kikanisa wako pamoja tayari na Yesu (Jh,17,22).Majina yao yameandikwa katika umoja usio gawanyika wa Kanisa la Mungu.Walifia dini kwaajili ya upendo ambao sasa wanaishi katika Yerusalem mpya karibu na mwanakondoo (Uf 7,13-17). Maisha yao waliyo toa sadaka , yanatulika  katika  ushirikiano na kutembea njia moja kulelekea umoja, mi kama vile Kanisa la kwanza kwa  wafia dini ambao wamekuwa mbegu mpya ya ukristo , na kwa njia hiyo hata leo damu ya wafia dini iwe mbegu kwa wote na chombo cha ushirikiano na amani.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.