2017-01-26 15:51:00

Umoja wa kweli unatokana na kujifunza kutoka kwa wengine


Kitendo cha Mtakatifu Paulo kukutana na Yesu njiani akielekea  Damasko , ilibadilisha maisha yake kabisa.Tangu wakati ule na kuendelea alitambua kwamba kuishi kwake hakutegemei na uwezo wake tu mwenyewe kwa kufuata sheria,bali  ni kutoka kwa nguvu zake zote na upendo wa Mungu bila kikomo,kwa njia ya Yesu Kristo msulibiwa na mfufuka.Hivyo ndiyo  kutambua maisha mapya yanayotokana na Roho ya kwamba nguvu ya Bwana mfufuka , inafanya uzoefu wa msamaha, uaminifu na kutia moyo. Paulo hawezi tena kubaki kimya juu ya habari hii , Kwa msukumo wa nguvu za Roho Mtakatifu anakwenda kutangaza habari njema  ya upendo na  maridhiano ambayo Mungu kwa njia ya Kristo anaitoa kwa binadamu.

Ni sehemu ya mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa masifu ya Jioni kusheherekea sikukuu kuongoka kwa Mtakatifu Paulo inayoendena sambamba na hitimisho la wiki ya maombi kwaajli ya umoja wa wakristo iliyoanza 18-25 Janauari 2017,katika Kanisa kuu la Mtakatifu Paulo nje ya kuta za Roma. Anasema maridhiano ya binadamu na Mungu kwa upande wa Mtume wa mataifa ,kwasababu yeye  amekuwa Balozi (2Kor  5,20) ni zawadi itokanayo kwa Kristo. Inajionesha wazi kutoka katika Barua ya pili ya Mtakatifu Paulo kwa Wakorintho ambayo ndiyo imeongoza kauli mbiu ya wiki ya maombi kwaajili ya Wakristo, ya kwamba Upendo wa Kristo unatuwajibisha  katika mapatano(2Kor 5,14-20).

Huo ni upendo wa Kristo na siyo upendo wetu kwa Kristo bali upendo wa Kristo alio nao juu yetu.Wakati huo huo , mapatano ambayo tunawajibishwa , siyo rahisi tu  kwa utashi wetu  bali ni mapatano hawali ya yote ambayo Mungu anatoa zawadi kwa njia ya Kristo.Ni yeye anaye kuja kwa njia hiyo kwani Baba Mtakatifu anaeleza,ni zawadi ya bure ambayo Mungu anatoa kabla ya kuwa na msukumo wa binadamu anaye amini na kutafuta kushinda mgawanyiko.Matokeo ya zawadi kwa mtu, aliyesamehewa na kupendwa , ameitwa kwa mara nyingine tena , kutangaza Injili ya mapatano  kwa maneno na matendo , ili aweze kuishi na kutoa ushuhuda wa uwepo wa mapatano.

Kwa mtazamo wa mgawanyiko kati ya wakristo , Baba Mtakatifu anasema tunaweza kujiuliza  swali hili tunawezaje kuhubiri Injili ya mapatano baada ya muhongo wa mgawanyiko? Jibu lenyewe linatoka kwa Mtakatifu Paulo mwenyewe, Baba Mtakatifu Francisko anasema kwa  Paulo anatusaidia kupata njia kwani Yeye mwenyewe anabainsha ya kwamba mapatano hayawezekani bila kuwapo kujitoa sadaka. Yesu alitoa maisha kwa kufia msalabani kwaajili ya wote. Kwa  mfano huo hiyo pia ni sawasawa na mabalozi wa mapatano ambao wanaitwa kwa jina leke kujitoa maisha , hao wasiishi kwaajili yao binafsi , bali kwa ajili ya aliyekufa na kufufuka kwaajili yao.(2Kor 5,14-15).Kama vile Yesu anavyofundisha ya kwamba ni pale tunapopoteza maisha kwaajili ya upendo  wake , Maihsa hayo tutarudishiwa tena kwa hakika (Lk 9,24). Baba Mtakatìifu anaeleza kwamba hayo ndiyo mapinduzi aliyoishi Paulo , lakini ni mapinduzi ya kikristo daima: siyo kuishi tena binafsi , kwaajili ya manufaa yetu , na kwa sifa, bali kwaajili ya sifa na utukufu wa Kristo kwa njia ya ke , pamoja naye , na upendo  wake na ndani ya upendo wake.

Baba Mtakatifu anasisitizia kuondokana na kushikila sheria zaidi akitoa wito kwamba kwa Kanisa na  kwa kila dhehebu ya Kikristo, ni mwaliko wa kutokushirikilia mipango, kuhesabu  na faida ,  na wala kutegemea fursa na mienendo ya kisasa bali ni kujaribu kutafuta njia , na kuangalia daima, msalaba wa Bwana kwasabuvu mbele ya msalaba ndipo ipo mipango yetu yote  ya maisha.Halikadhali ni wito wa kuondoka na aina kujibagua na kushinda vishawishi vya kujiona ambapo uzuia kupokea kile ambacho roho Mtakatifu anatenda  njema ndani  ya maisha yetu. Mapatano ya kweli kati ya wakristo yatawezekana tu iwapo tukiweza kutambua tunu walizo nazo wengine , au kuwa wapole na uwezo wa kuwa wanyenyekevu, kujifunza kutoka kwa wengine , bila kusubiri wengine wajifunze kutoka kwetu.Hivyo Baba Mtakatifu anasema tukiishi hivyo na kufa sisi wenyewe  kwaajili ya Yesu, mitindo ya kizamani ya kuishi itafungua na kufunika wakati uliopita na kufanana na yule Mtakati Paulo yaani wa kuingia katika mtindo mpya wa kuishi kwa umoja.

Kwa pamoja na Paulo tunaweza kusema “Mambo ya zamani yamekwisha (2Kor 5,17). Hata hivyo kutazama  nyuma no muhimua kwani inasaidia kusafisha kumbukumbu , lakinini kushiklia ttu mapito kwa kukaa na kukumbuka mabay yaliyojitokeza au kupokea ,na kuhukumu kwa mtazamo tu wa kibinadamu, unaweza kugandamiza na kuzuia kuishi wakati uliopo. Neno la Mungu linatia moyo  wa kupata nguvu  kutoka katika kumbukumbu, na kukumbuka mema tuliyoyapokea kutoka kwa Bwana.Baba Mtakatifu anasema kwamba  lakini hiyo inatuwajibisha  tuache nyuma yetu wakati uliopita kumfuata Yesu  leo hii. Na kuishi kwa mara nyingine tena na Yeye.Tumruhusu Yeye afanye kila kitu kipya (Uf 21,5) na kuwa na mwelekeo endelevu , unaofungua matumani yasiyo danganya kamwe , matumaini endelevu ambayo yaweza kushinda mgawanyiko wa waamini, walio geuka wapya katika upendo , na watakuwa hakika  wanaonekana katika umoja.

Akikumbuka maadhimisho ya miaka 500 ya waluteri,  Baba Mtakatifu anasema wakati tukiendelea  katika njia hii ya umoja , mwaka huu tunakumbuka kwa namna ya pekee ya miaka 500 ya mageuzi ya kiprotestanti. kitendo leo hii cha wakatoliki na waluteri kukaa pamoja na kufanya kumbukumbu , ni tukio la mgawanyiko wa Wakristo uliojitokeza wakati ule, na hivyo tuwe na matumaini , tukimweka Yesu mbele  kwa tendo lake la mapatano, ni tendo kubwa , ambalo kwa neema ya Mungu na sala , kupitia miaka 50 ya kutambuliwa kwa mazungumzo ya kiekumene.Pamoja na hayo baba Mtakatifu anatoa salam zake za pekee kwa kiongozi Gennadios , wawakilishi wa kipatriaki wa kiekuemene, Grazia David Moxon, mwalikishi wa Roma Askofu Mkuu wa Catentebury , na  wawakilishi wote kutoka makanisa mbalimbali  kwa ajili  ya mazunguzo ya taalimu Mungu kati ya Kanisa na makanisa ya kiotodosi mashariki ya mbali, akiwatakia kazi yenye kuleta matunda mema  katika mkutano  wao wa mwaka unaondelea kwa siku hizi mjini Vatican.
Pia aliwasalimia wanafunzi wa  chuo cha kiekumeni cha Taalimungu huko Bossey, ambao wako Roma kwaajili ya hija ya mafunzo  na utambuzi wa Kanisa Katoliki. Vile vile vijana wa Kiorthodox na Waorthodox wa Makanisa ya Kiorthodox wanaosoma Roma.


Na mwisho Baba Mtakatifu anakumbuka kusali kwa ajili ya wote na hasa zaidi wanaoteseka akisema: Sala yetu  kwaajili ya umoja wa Wakristo imetanguliwa na sala ya Yesu aliyo mweleza Baba yake  wakati wa mateso akisema ,” Ili wote wawe na umoja”(Yh17,21).Tusichoke kamwe kuomba  kwa Mungu zawadi hiyo,kwa uvumilivu na kuamini , ni mategemeo ya kwamba  Bwana amjalie kila mwamini wema wake wa umoja uliojaa na kuonekana,uendelee  kutoa  ushuhuda   wake kwaajili  ndugu zetu ,ambao jana na leo wanazaidi kuteseka kwa ajili ya Jina la Yesu, tutambue kwamba kila fursa ambayo tunapewa  ni fursa nyeti ya  kusali kwa pamoja , kumtangaza Yesu , kumpenda , kumtumikia pamoja na zaidi kwa  masikini na wa pweke.

Sr Angela Rwezula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.