2017-01-26 16:05:00

Mapatano ya Wakristo yanawezekana kwa sababu ni utashi wa Mungu


Mara baada ya Masifu ya Jioni katika sikukuu ya Kuongoka kwa Mtakatifu Paulo Mtume wa mataifa , katika Basilika ya Mtakatu Paulo Kardinali Kurt Koch Rais wa Baraza la Kipapa la Umoja wa Wakristo alitoa salamu zake  kwa Baba Mtakatifu Francisko  , ikiwa pamoja na kufunga wiki ya maombi kwaajili ya Wakristo kwa mwaka 2017 .


Kardinali anasema kuadhimisha haya masifu ya Jioni katika sikukuu ya Kuongoka kwa Mtakatifu Paulo , anapenda kutoa salam zake, kwa niaba ya ndugu wote  waliounganika  ndani ya Basilika ya Mtakatifu , akimshukuru, uwepo wake wa kupendelea kwa mara nyingine tena mwaka huu kuwa pamoja nao, akikimbuka , shughuli zake kuhusu, suala la kiekumene katika umoja  wa wakristo ambao Kardinali anasema Baba Mtakatifu ameweka kipaumbele katika utume wake.Wiki ya maombi kwaajili ya Umoja wa Wakristo inayomalizika , anasema  imeongozwa na maneno ya Barua ya pili  ya Mtakatifu Paulo kwa Wakorinto kwa kauli mbiu “upendo wa Kristo  unatuwajibisha katika mapatano!.

Kauli mbiu hiyo ilichaguliwa na Jumuiya ya makanisa ya Kikristo wa Ujerman, wakiwa wanatambua vema ya kwamba historia ya mageuzi , iliyoanza miaka 500 iliyopita, na ambayo inaadhimishwa kwaka huu. Hiyo historia inajikita siyo tu  ugunduzi wa Injili na neema za bure kutoka  kwa Mungu , bali hata utambuzi wa machungu ya mgawanyiko ulijiokeza , amabao kwako Baba Mtakatifu,ulikumbuka  pamoja ukiwa na Rais wa Shirikisho la kiluteri duniani.Askofu Younan, wakati wa kusaini mkataba wa pamoja wa Lund , kwa maneno haya: “Tukiwa tunamshukrur Mungu kwaajili ya zawadi za kiroho na kiteolojia tulizopokea kwa njia ya mageuzi, tunakiri na kulaani mbele ya Kristo, kitendo cha waluteri na wakatoliki kuumiza umoja unaonekana wa Kanisa “


Kukiri na kusafishwa ,ni kumbukumbu ya kihistoria ambayo inapaswa kuonekana , kwa ajili ya ishara ya mapatano ambayo inawezakana tu iwapo Mungu mwenyewe ndiye mwanzilishi.Kwani inawakilisha zawadi ambayo Mungu anafanya kwaajili ya binadamu , na kwaajili ya ulimwengu mzima.
Ili kuwa na mapatano kwa Mungu katika Kristo , hatuna budi sisi wenyewe kufanya kwanza mapatano na Bwana tunapaswa kuwajibika , katika kuhamasisha mapatano kati ya wakristo na kuacha msukumo wa upendo wa kwaajili ya Kristo uingie ndani mwetu, kwani upendo hakika ndiyo injini yak ila nguvu yoyoyte ya kiekumeni.Lakini upendo wa kweli hauti yale matukio yote yaliyokea kati ya makanisa ya Kikirsto, bali upendo unatupeleka twenda pamoja kwenya mapatano ya kina.Ni upendo  wa Yesu unaotuwajibisha katika mapatano na hivyo  tutambue ya kwamba ujumbe huo  ndiyo lengo kuu  la wajibu wa kiekumene,kwajili ya Baba Mtakatifu na kwaajili ya Umoja wa wakristo.

Halikadhalika Kardinali Kurt anatoa shukrani za dhati kutoka moyoni mwake kwaajili ya ushuhuda wa Baba Mtakatifu Francisko akitoa ahadi ya kumsindikiza katika sala zale kwaajili ya utume wake kama khalifa wa mtume Petro katika kujenga madaraja na katika mapatano kati ya wakristo,na mwisho anaomba Baraka kutoka kwa Baba Mtakatifu. 

 

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.