2017-01-26 08:36:00

Fra' Mathew Festing "abwaga" manyanga!


Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 24 Januari 2017 alikutana na kuzungumza kwa kina na mapana na Fra’ Matthew Festing na hatimaye, kukubali kung’atuka rasmi kwa Frà Festing kama Kiongozi mkuu wa Jeshi la Malta kuanzia tarehe 25 Januari 2017. Baba Mtakatifu anampongeza na kumshukuru kwa kuonesha uaminifu wake kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro pamoja na unyenyekevu wake wa kutaka kuendelea kuhudumia ustawi na maendeleo ya Jeshi la Malta na Kanisa katika ujumla wake. Katika kipindi hiki cha mpito, uongozi wa Jeshi la Malta ambali limekuwa mstari wa mbele katika kulinda na kushuhudia imani, utakuwa chini ya Kamanda mkuu, huku wakiendelea kusubiri uteuzi utakaofanya na Baba Mtakatifu mwenyewe hapo baadaye!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.