2017-01-23 17:01:00

Tuone maajabu ya ukuhani wa Yesu na tukubali kusamehewa na Mungu


Ni maajabu makubwa ya  ukuhani wa Yesu kristo aliyejitoa mwenyewe , mara moja hata milele kwaajili ya msamaha wa dhambi,na sasa anatuombea sisi mbele yake, Yeye   atakuja tena kutupeleka kwake Mungu Baba. Ni hatua tatu za maajabu ya ukuhani wa Yesu Kristo ambao umejitokeza katika mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko katika Kikanisa cha Mtakatifu Martha kilichoko mjini Vatican, Jumatatu 23 Januari 2017. 

Mahubiri ya Baba Mtakatifu yametokana na somo la kwanza kutoka katika kitabu cha Waebrania , iliyohusu Kristo kuwa mpatanishi wa Agano  ambalo Mungu nafanya na watu,anafafanua kuhusu hatua  hizo akisema; Hatua ya kwanza ni kujitoa mwenyewe ; wakati makuhani wa gano la kale walikuwa wakitoa sadaka ya kafara , Yesu Kristo alijitoa mara moja na milela kwaajili ya msamaha wa dhambi na kwa majabu hayo ni yeye alitupeleka kwake yeye Baba na yeye ameutengeneza ule uhusiano wa kazi ya uumbaji.Hatua ya pili ya maajabu ni ile ambayo Bwana anatenda  mwenyewe, yaani anasali  kwaajili yetu, tunaposali hapa na yeye anasali kwaajili ya kila mmoja wetu , akisema mimi ninaishi na niko mbele ya Baba ninaomba , ili imani yetu isipungue. Baba Mtakatifu anasema mara ngapi mapadre wanaombwa kusali , kwababu sala ya mapadre ina nguvu zaidi wakati wa sadaka ya misa altareni.

Na hatua ya tatu ya maajabu  ni ile ambayo Yesu mwenyewe atarudi tena, lakini kwa mara hii ya tatu, haikutakuwepo  uhusiano wa dhambi , bali itakuwa  ni ukamilifu wa ufalme wa mbingu, ambapo  atatupeleka kwa Baba .Kuna maajabu makubwa katika ukuhani wa Yesu  katika hatua tatu, kwasababu anasemehe dhambi mara moja da daima, anasali kwaajili yetu na atakaporudi tena ,Lakini Baba Mtakatifu anabainisha kwamba  pamoja na hayo kuna kinyume cha kutokusamehe  na hiyo ni ngumu kumsikia Yesu akisema mambo hayo , lakini yeye anasema , na kama yeye  anasema ni kweli. Tunatambua kwamba Bwana anasemehe yote na hasa tunapumfunulia mioyo yetu.Na hata dhambi yoyote iliyo kubwa inasamehewa, lakini ni dhambi tu ya kukashfu  Roho Mtakatifu ambayo haitasamehewa kamwe.

Kwa kuelezea hiyo Baba Mtakatifu anaelezea juu ya mpako wa ukuhani wa Yesu  ya kwamba ni Roho mtakatifu alimshukia Bikira Maria na vilevile Makuhani wakati wa kupata daraja la upadre wao wamepakwa mafuta matakatifu: Na hivyo Hata Yesu akiwa kuhani Mkuu alipokea upako huo. Je huo ndiyo ulikuwa mpako wa kwanza? Baba Mtakatifu anajibu hapana, bali  hata katika mwili wa Bikira Maria  kwa uwezo wa Roho Mtakatifu .Na kwa njia hiyo anayetoa kashfa juu ya msingi  wa upendo wa Mungiu ambao ni ukombozi na uumbaji , ni kukashfu ukuhani wa Kristo.Baba Mtakatifu anasema unaweza kufukiri Bwana ni mbaya , lakini hapa Bwana anasamehe yote , na  kwa yeyote anayesema mambo hayo anafunga msamaha  na hataki kusamehewa wala kujiachia  kusamehewa.

Baba Mtakatifu Francisko anasema na hiyo ni mbaya kukashfu Roho Mtakatifu , ambapo hutaki kusamehewa kwasababu umekana ukuhani wa Yesu aliyefanyika kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.Kwa kumalizia Baba Mtakatifu anarudi tena katika maajabu makubwa ya  ukuhani wa Kristo na kutokusamehewa dhambi kwaajili ya kashfa , akisema siyo kwamba Bwana hataki kusamehe yote bali ni kwasababu huyo aliye toa kashfa  amejifunga kiasi cha kutokukubali msamaha dhidi ya kutoa kashfa ya maajabu ya Yesu.

Leo hii itakuwa vizuri wakati wa madhimisho ya misa, kufikiria mbele ya Altare kwamba  tunafanya kumbukumbu hai, kwasababu yeye yupo na yeye ndiye kuhani wa kwanza Yesu aliyejitoa maisha yake kwaajili yetu . Vilevile kuna kumbukumbu  hai ya ukuhani wa pili kwasababu yeye anatuombea hapa katika misa hii na  tutakaposali sala ya Baba yetu  na hatua ya tatu ya ukuhani wa Yesu , ni kwamba atakuja tena , yeye ni matumaini yetu na utukufu  na hivyo  tuombe neema ya Bwana kwamba mioyo yetu kamwe isifungwe katika maajabu haya na ya ukarimu mkubwa kwetu.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.