2017-01-23 15:18:00

Rais Erdogan wa Uturuki anatembelea: Tanzania, Msumbiji na Madagascar


Rais Recep Erdogan wa Uturuki amewasili nchini Tanzania Jumapili, Januari 22, 2017 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere na kupokelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na niaba ya Mheshimiwa Rais. Dkt. John Magufuli.

Rais huyo ameambatana na mkewe Mama Emine Erdogan pamoja na Mawaziri watatu ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa Mevlüt Çavuşoğlu,Waziri wa Uchumi Mheshimiwa Nihat Zeybekekci na Waziri wa Nishati na Maliasili Mheshimiwa Berat Albayrak. Pia Rais huyo ameambatana na wafanyabiashara wapatao 85 wa nchi hiyo. Hii ni ziara inayopania kuimarisha uhusiano kati ya nchi ya Uturuki na nchi kadhaa barani Afrika. Katika ziara hii ya kikazi,  Rais Erdogan anatembelea pia Msumbijina Madagascar.

IMETOLEWA NA

OFISI YA WAZIRI MKUU.








All the contents on this site are copyrighted ©.