2017-01-23 15:40:00

Baba Mt. Francisko kuwatia moyo wanaopambana na vitendo vya kihalifu


Jumatatu 23 Janauari 2017 Baba Mtakatifu Francisko alikutana na wawakilishi wa uongozi wa Kitaifa wa Italia  wanaopambana na vitendo vya uhalifu na kigaidi, akisema, mmekabidhiwa kufutia shughuli  katika sekta kubwa wa waarifu wa makundi ya aina tatu  yenye kujulikana  kama: mafia, camorra na ndrangheta. Wao wanalenga kunyonya udhaifu kiuchumi, wa kijamii na kisiasa,katika sehemu hizo  wanapata eneo lenye rotuba ili kukamilisha mipango yao.Pamoja na ujuzi mlionao mnakumbana pia na vikosi vya kigaidi vinavyo endelea kusambaa  kila kona. Baba Mtakatifu anawapongeza kwa juhudu hizo na kuwatia moyo katika kazi hiyo ngumu na hatarishi, ambayo ni muhimu kuwaokoa watu kuondoka na  utawala wa hayo makundi ya kiharifu ambayo yanasabisha vurugu , na umwagaji wa damu.

Jamii inahitaji kukombolewa dhidi ya rushwa  biashara haramu ya madawa ya kulevya na silaha, usafirishaji wa binadamu, wakiwemo watoto  ambao wamefanywa watumwa.Haya yamekuwa hakika madonda ya kijamii na wakati huo pia ni changamoto ya ulimwengu, ambapo kwa pamoja kimataifa wanapaswa kukabiliana na kutoa uhamuzi.Kwa mtazamo huu, nimejifunza Baba Mtakatifu anasema kwamba, shughuli  zenu za utekelezaji wa kisheria mnazofanya kugundua wahalifu, mnaifanya ipasavyo kwa kushirikiana  na wenzenu katika mataifa mengine.Kazi hiyo ufaninyika  kiharambee  kwa kutumia vyombo vyenye kuleta ufanisi katika usalama kwa jamii ya pamoja.

 Anasema, Serikali hutegemea sana taaluma yenu na uzoefu wa mahakimu wanaojikita katika uchunguzi wa kupambana na kukomesha uhalifu uliopangwa.Ninawasihi kujishughulisha kwa kila juhudi katika kupambana na na kukomesha biashara ya kusafirisha watu na magendo ya wahamiaji.Huo ni uhalifu unao kithiri nakuwaathiri wale wadhaifu zaidi. Kwa suala hili ni muhimu kuongeza kazi ya kuwalinda waathirika, ikiwa ni pamoja na msaada wa kisheria na kijamii kwa ajili ya ndugu zetu wanaotafuta amani kwa siku zijazo. Ni wale wanaokimbia nchi zao kwasababu ya vita, vurugu , mateso, ambapo   wanayo haki ya kupata ulinzi katika  nchi zinazojiita ni za kijamii.

Kwa kushirikiana na kuimarisha kazi yenu yenye thamani kwaajili ya wale wanaokandamizwa, inabidi kutafuta namna ya kuingiza elimu hasa kwa upande wa kizazi kipya. Kwa lengo hili , Mashirika mbalimbali  na Taasisi kama vile za familia, shule, jumii ya kikristo, michezo na utamaduni wanaalikwa kukuza ufahamu wa maadili na mwongoz wa maisha ya uaminifu, amani na umoja , ambao kwa hatua unaweza kushinda maovu na kusafisha njia katika wema.Na hii ni lazima kuanzia katika dhamiri, ili kupata kurejesha nia kuchagua , mitazamo ya mtu binafsi , na hivyo jamii nzima inawza kuwa wazi kwa matumanini ya ulimwengu.Tukio la Mafia ni usemi wa utamaduni wa kifo , na hivyo inabidi kuupinga.Kwa kiasi kikubwa ni kuonesha imani ya Injili ambayo daima inakazia maisha.Wale wanomfuata Yesu  mawazo yao  ni amani, undugu, uadilifu , kukubalika na msamaha. Mtitirko wa Injili ukijikita ndani mitume wa Yes, ukoma na kuzaa  matunda mema, yanayotambulikana hata kwa nje, kwa tabia na mwenendo , ambayo Mtakatifu Paulo alifananisha na "upendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu, upole, na kujiamini mwenyewe.” (Gal 5,22).

Aidha Baba Mtakatifu anasema , anafikiri parokia nyingi na vyama katoliki ni mashihidi wa matunda hayo.Wao wanatenda shughuli hizo kwa lengo la kuhamasisha watu na kukuza utamaduni ambao hatua kwa hatua wanaweza kutokomeza  mizizi  iliyopandwa na wahalifu na wala rushwa. Katika juhudi hizi ,pia Kanisa linaeonesha ukaribu wake kwa wale wanaoishi  katika hali hiyo na ili wapate kuondokana na vurugu hizo kwa matumaini.Baba Mtakatifu anawatakia  Baraka za Mungu Baba ya kwamba awape nguvu za kuendelea mbele , na kutokukata tamaa , bali kuendelea katika kupambana na vurugu za Mafia na Ugaidi. Yeye anatambua kwamba kazi yao ya utekelezaji hubeba hatari  ya maisha au athari nyingine kwaajili ya famila zao, na kwa njia hiyo inahitaji kuongeza utashi na ujasiri wa wajibu wa kazi. Mwishoni, Baba Mtakatifu aliomba Huruma ya Mungu , iwaguse mioyo ya watu hao waharifu wa aina zote za mafia waache kutenda mabaya, na waongoke na kubadili maisha  akisema fedha  chafu, biashara na uhalifu wa mafia ni fedha za damu na inazalisha nguvu isivyo haki.Alimalizia Baba Mtakatifu Francisko.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican 








All the contents on this site are copyrighted ©.