2017-01-21 15:29:00

Mkutano wa amani kwa ajili ya nchi ya Syria huko Astana


Jumatatu 23 Januari 2017 utafunguliwa mkutano juu ya amani ya Syria huko Astan mji Mkuu wa Kazakhstan.Wanaotarajiwa kudhuria mkutano huo ni pamoja na wawakilishi kutoka nchini Urusi na Marekani, na pia uwepo wa mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa Bwana Staffan De Mistura. Pamoja na hayo taarifa zinasema kwamba bado wanaendelea na mapambano katika maeno ya Palmira kutokana na jeshi la kijihad na Isis ambao wameharibu sana sanaa nyingi na muhimu, hadi Shirika la UNESCO kutamka kwamba ni uharifu wa vita.

Mwandishi wa Radio Vatican Roberta Barbi alimhoji Profesa Alberto Ungari mkufunzi wa Historia ya nadharia na vitendo ya kisiasa, Luiss Roma kuhusiana na mkutano huo juu ya amani.Yeye alisema kwa hakika upo utashi kwa sehemu zote za kutafuta suluhisho kwasababu ya dharura ya Syria japokuwa wana husika siyo peke yao tu kwa upande wa Ulaya bali ni kwa  sehemu zote za dunia: na hivyo ni hali ambayo kwa hakika,inapaswa kupata ufumbuzi wake,pamoja na uwepo wa mabadiliko katika urais Marekani unaweza pengine kuwezesha utatuzi wa suala hilo.

Mwandishi wa habari aliuliza akisema kwa mujibu wa Rais Assad, huenda kuna uwezekano wa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya sehemu zote na kipaumbele kitakuwa ni kusitisha mapigano kinadharia iliyokuwa imetangazwa tangu 30 Desemba 2016.Profesa Ungari alijibu akisema; kusitisha mapigano ki ukweli hawakuheshimu, kwa pande zote za nchi  kama ilivyokuwa imetangazwa. Kusitisha mapigano hayo ilikuwa ni mojawapo ya misingi wa mikataba mingine ambayo ilikuwa imetolewa tangu mwanzo chini ya Urais wa Obama, na ambayo haikuchukua muda mrefu. Kwa maana hiyo tunategemea kwamba inawezkana ikawepo dhamira kuu ya ufanisi wa Mkutano huo,na hiyo itakuwa kwa wale watendaji ya mifumo yote ya kisiasa walioko katika maeneo.

 Aidha akijibu swali juu ya uwepo wa mwakilishi maalumu kutoka Umoja wa mataifa  De Mistura una maana gani , Profesa anasema kwamba, De Mistura ameripotiwa mara nyingi akijaribu kwa kila njia  kurekebisha hali ya kisiasa ya Syria. Hivyo ni dhahiri kwamba uwepo wake ni muhimu kwani  unatoa mamlaka katika mazungumzo ya amani  na pia uwepo wake ni kama  ishara  ya mwelekeo wa maamuzi ya Umoja wa Mataifa , ambapo kwake hatimaye wanaweza kufikia utatuzi wa hali hiyo tete na  ambayo kwake binafsi anasema imeathiri sana katika ukosefu wa utulivu wa maeneo yote na zaidi katika maeneo hatari kama vile Jordani na Libanon. Hivyo siyo nchi ya Syria tu , anasema Profesa , bali ni  kuhusu kujenga hali ya utulivu mkubwa katika maeneo yote ya Mshariki ya kati na changamoto zote zinazojitokeza hasa kwa idadi kubwa ya wahamiaji na kwa upande wa Ulaya.

 

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.