Familia na changamoto zake ndiyo imekuwa kiini cha mkutano wa Kamati ya Baraza la maaskofu wa Rwanda kwaajili ya familia na Kanisa nchini humo.Habari kutoka katika mtandao wa Baraza la maaskofu wa Rwanda (Cepr) zinasema Kamati hiyo imekutana hivi karibuni mjini Kigali , na kungozwa na Askofu Antoine Kambana, Askofu wa Jimbo la Kibungo na rais wa Kamati hiyo.
Wakati wa kazi ya kikao chao, waliteua kamati ndogo sita , na kila kamati iweze kuwajibika
kwaajili ya kuchambua kila changamoto juu ya maadili ya ngono na familia, afya,vijana,wanafamilia
kusindikizwa,sheria,na maadili mpya ya dunia.Mihimili mpya hiyo kwa sasa inapaswa
kufanya kazi juu mpango wa mikakati mitano,kwaajili ya tume ili kukabiliana na mambo
mengi kama vile itakadi ambayo inaweza kuharibu familia.Wanatoa mfano kwamba kuna
baadhi ya mipango ya mafundisho inayotolewa kwa mtazamo rahisi utafikiri ni muhimu
na yenye manufaa , na kumbe ni kinyume kwani kuna vipengele vinavyopingana na maadili
ya familia.
Pamoja na hayo Mkutano huo ulikuwa pia na hoja ya maandalizi ya wiki ya familia ambayo
inatarajiwa kufanyika kuanzia 13-19 Februari 2017. Nia ya maandalizi hayo ni kutaka
kuhamasisha hisia na kutoa umuhimu wa familia, mahitaji yake ya haraka,kwenye usimamizi,
thamani yake ya ndoa ya familia.
Aidha wameafikiana kufanya wiki hiyo wakati wa tukio la sikukuu ya Mtakatifu Valentine
ifanyikayo kila mwaka 14 Februari ili kuwawezsha kuhamasisha zaidi wakristo katika
kuonesha upendo wa kweli na dhati wenye maana, ambapo kila parokia watatakiwa kuandaa
mpango maalumu na wakati huo Baraza la maaskofu watatoa ujumbe wa siku hiyo.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |