Mafundisho ya dini katoliki katika nchi ya Italia ni somo linalopendwa na vijana kwa asilimia 80% ya wanafunzi ambapo imeonesha kiwango cha asilimia kubwa hiyo kutokana na takwimu za Taifa kuonesha juu ya ufundishaji wa somo hilo la dini katoliki. Aliyatamka hayo wakati wa kutoa toleo jipya la kufundishia Jumanne 17 Januari Roma na Rais wa Baraza la Maaskofu Italia,Askofu Nunzio Galantino.
Mafundisho ya dini shuleni limechaguliwa sana na wanafunz kwani alisema kwani katika
utafiti wa kitaifa inaonesha kwamba wapo walimu 3,000 wanao fundisha somo la Dini
Katoliki na zaidi ya wanafunzi 20,000 wana udhuria katika somo hilo.Lakini pia askofu
anasema kwa miaka iliyopita ilionesha kushuka kwa kiasi japokuwa haikushuka sana.Pamoja
na hayo inaonesha asilimia 91,7% ya wakufunzi wa somo hili wako katika shule za Serikali
na asilimia 56% wanafundisha katika shule Katoliki, licha ya hayo wanao udhuria
somo la dini Katoliki ni wote hata wale wasio wakatoliki.
Askofu Galantino anasema; wakati mwingine somo hili la mafundisho ya dini katoliki, uonesha kupuuzwa na sehemu ya jamii, hiyo ni kwasababu ya dunia hii tunamoishi ambapo kumekuwa na itkadi mbalimbali ambapo utoa ushawishi wa kutupilia hewani kila kitu,ambacho hadi sasa kimetendeka. Pamoja na yote askofu anaeleza kuna jambo la kutia moyo kwa ufundishaji wa dini na hasa kuona kwamba asilimia 67%ya walimu wanaofundisha somo hili na wanatoa maana ya maisha kwa vijana na zaidi ya asilimia 57% wanaunga mkono kwamba hii inasaidia katika kukabiliana na utamaduni.
Askofu Galantino pia anasema udhaifu wa somo hili la dini ni kutojua kutofautisha kati ya mafundisho ya dini na katekisimu , pamoja na kwamba asilimia 96% ya walimu ni walei .Alimazia akisema , mafundisho ya somo la dini katoliki au mafundisho ya katekisimu siyo lengo katika shule za Umma za Italia,bali narudia kusema mafundisho ya dini katoliki ni mafundisho yanayo jikita kikamilifu katika mtaala wa shule , na kujikita kikamilifu katika hali ya utamaduni wa jamii ya Italia.
Sr Angela Rwezaula.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |