Jumanne 17 Januari 2017 ,umefunguliwa Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi mjini Davos
, Uswis, ambao ni mkutano wa 47 wa Kimataifa, na kwa mara ya kwanza Rais wa China
Xi Jinping alipata kuhudhuria na kuhutubia juu ya marekebisho yanayopaswa kufanywa
na utandawazi. Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi unategemea kumalizika Ijumaa 20 Januari
2017
Mkutano huo umewakilishwa na watu 3000 wakiwa ni Wafanya biashara , viongozi wa Umoja
wa Mataifa, pamoja na wanaharakati na wataalamu kutoka nchi 70 wakiongozwa kwa
kauli mbiu “uongozi katika kuwajibika”, wanapanga kujadili masuala moto moto ya sasa
ya kimataifa yanaohusu mambo ya kiuchumi, na kisiasa, na mada inayohusu suala la kukosekana
kwa usawa na maendeleo ya kiteknolojia ambayo yanasababisha kupungua kwa nafasi za
ajira.
Katika hotoba yake Rais wa China, Xi Jinping, alisema China inakaribisha uwekezaji
wa kigeni; na kuonya dhidi ya kuzuka kwa vita vya kibiashara,na pia katika mkutano
huo alitoa tahadhari kuwa vita vipya vya kibiashara havita saidia maslahi ya upande
wowote, na kufuata sera ya kulinda viwanda vya nchi kwamba italeta matokeo mabaya
akitoa mfano na kusema "Kutafuta ulinzi wa soko la ndani ya nchi ni kama kujifungia
mwenyewe katika chumba cha giza. Ingawa utakuwa unajilinda dhidi ya upepo na mvua
vinavyoendelea nje, lakini pia utakuwa unajinyima mwanga na hewa. Hakuna mtu itakayeibuka
mshindi katika vita vya biashara," alisema Xi Jinping.
Ikumbukwe kwamba hii ni kwa mara yake ya kwanza kwa kiongozi wa China ambalo ni
taifa la pili kwa ukubwa kiuchumi baada ya Marekani; kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa
wa Uchumi unaofanyika kila mwaka mjini Davos, Uswis, na kwa njia hiyo amepata kwake
fursa kama Rais kujaribu kuionesha China kama kiongozi wa kupambana na sera ya kulindwa
kwa viwanda vya nchi na mtetezi wa utandawazi duniani, kwa njia hiyo alisema kwamba
ataendelea kuweka mlango wazi kwa biashara na hataufunga.
Na Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |