2017-01-16 14:34:00

Urbanczyk:Tunayo changamoto ya kupunguza matatizo na migogoro


Amani ndiyo iwe ajenda ya kikao cha 1127 cha mwaka katika Baraza la OSCE, hayo yalitamkwa na mwakilishi wa Vatican, katika Baraza la kudumu la OSCE Monsinyo Janusz Urbanczyk  wakati wa Mkutano wao wa mwaka  huko Vienna 12 Januari 2017.
Monsinyo Janusz alianza hotuba akimkaribisha , Waziri wa Mambo ya nchi za Nje wa Austria Bwana Sebastian Kurz katika Shirikisho la umoja wa nchi za Ulaya kurudi kwa mara nyingine tena katika Baraza la kudumu, kwasababu ya kuchukua nafasi ya wenyeji  wa  kukaribisha vikao vya OSCE kwa mwaka 2017 nchini Austria.Na alihaidi kwamba Vatican itakuwa na ushirikiano na kutoa  msaada kwa kipindi chote watakachokuwa wenyeji wa vikao vya  OSCE Austria.


Mwaka 2017 umeanza na kivuli cha migogoro mingi kutokana na mashambulizi ya kigaidi katika mikoa ya baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya kwa mwaka 2016.Ni lazima tukubali kwamba watu wengi wamekuwa na wasiwasi na kutambua vema juu ya matokeo ya migogoro , fitina na ugaidi, ambao unazua wasiwasi na hofu  kwa siku zijazo badala ya kujiamini kwa hisia za usalama.
Ili kuhakikisha, wasiwasi katika hali halisi unatoweka kwa ajili ya amani, ni lazima uwepo ushirikiano wa pamoja katika ajenda ya baraza letu. Vatican  iko tayari kusaidia juhudi  zitakazofanyika katika mikutano ya Austria kuwa mwenyeji ,kwa kutafuta  haraka mipango ya kupunguza matatizo  na migogoro   kwa uamninifu kati ya washiriki 57 kutoka mataifa mbalimbali ili kupambana na siasa kali na vikundi vyenye msimamo mkali.
Halikadhalika, Monsinyo Janusz anasema Vatican imeunga mkono  Baraza la mawziri huko Umburg iliyopitisha uamuzi juu ya wajibu wa OSCE kukabiliana na kipeo kikubwa cha wakimbizi na wahamiaji , watu wanaokimbia vita , manyanyaso  na mateso kama vile umasikini, ubaguzi, mambo hayo ni vipengele muhimu katika nchi zetu kwa miaka ijayo.


Aidha tunawapongeza Austria kuwa wenyeji  na kwa ahadi yake ya kuendelea na kasi iliyofanywa na Uswis , Serbia na Ujerman kuhusu wahamiaji, na wakimbizi wa ndani,hasa tangu wakimbizi wengi waingie kutoka mikoa ya MENA kutokana na ukosefu wa uhuru, ikiwa pamoja na uhuru wa dini au imani zao.Nchi zinazoshiriki zinapaswa kuhakikisha kwamba watu wote wanafurahia haki za binadamu, kama asemavyo Baba Mtakatifu Francisko.
Tunahitaji kuchua hatua dhidi ya vyanzo  na siyo madhara tu ya matukio, kwani sababu nyingi zingeweza kushughulikiwa wakati uliopita, na hivyo maafa na athari zake vingeweza kuzuilika.Monsinyo anasema lakini hata sasa kabla hatujachelewa kwa kiasi fulani tunaweza kutenda jambao  ili kumalizia majanga haya na kujenga imani.


Vilevile, Monsinyo  Janusz alipongea juhudi ya Mashirika mbalimbali kwa ushirikiano katika harakati za kuokoa watu  kwenye Kanda za Meditreanea, na kusema Baba Mtakatifu amekuwa akirudia wito juu ya mifumo  ya fedha na uchumi ya kwamba iweze  kuendeleza maendeleo ya binadamu  na kuhakikisha unakuwepo ulinzi  kwa huduma ya nyumba yetu kwa njia ya sera nzuri za kimazingira.Aidha aliendelea kusema changamoto ya  haraka tuliyo nayo  ni kulinda nyumba yetu  ya kawaida na pia kuleta familia nzima ya binadamu katika kutafuta maendeleo endelevu, ambapo tunajua kwamba madiliko yawezekana  . 

Kwa miaka 40 zaidi mradi mkubwa ulizinduliwa na kutiwa saini na Helsinki Final Act na Vatican inatoa msisistizo maalumu wa mwelekeo wa tatu wa kulenga haki za binadamu ili kulinda heshima ya binadamu wote , bila ubaguzi wa rangi ,jinsia , lugha au dini.Kwa jinsi hiyo Vatican inaunga mkono kutoa msaada kwaajili ya kuimarisha na kuweka vipaumbele kwa ujumla katika ukubwa wa binadamu kwenye Baraza la Osce ambalo limekuwa mwenyejiwake  Austrria .Munsinyo anasema kwamba Vatican inao uhakika kwamba chini ya usimamaizi OSCE  inawezekana kufikia makubaliano juu ya maazimio ya mawaziri wa Baraza juu ya kuimarisha juhudi za  kupambana na ubaguzi wa aina yoyote dhidi ya waislaim, wakristo na baadhi ya madhehebu madogo  kama vile mapambano dhidi ya ubaguzi wa wayahudi. 

 

Anatoa wito juu ya kuwapo na mazungumzo na ushirikiano ambao unaweza kukuza kujiamini kutokana na  maridhiano , kuheshimiana na kuelewana ,na hizo ndiyo njia za kufikia amani.Pamoja na juhudi hizo  Monsinyo Janusz ansema, bado kuna mambo mengi yana hitajika kufanywa ili kuendeleza kweli hali halisi ya usawa kati ya wanawake na wanaume kama vile kupambana na ukatili dhidi ya wanaweka , suala ambalo linazidi kuwa changamoto kubwa linalo athiri wanawake wengi , na kwa kiasi kkubwa ni ukiukwaji wa utu wao na haki msingi za binadamu.


Aidha mwakilishi wa Vatican anabainisha kwamba  jumuku la madaraka aliyo pewa na OSCE kuwa na ofisi zake Austria kwa mwaka 2017, kwa masuala muhimu  yaliyopitishwa  mwaka huu kwa kushirikiana , lazima  kutatuliwa. Na mwisho akiwatakia  mafaniko mema katika kukuza zaidi usalama na ushirikiano kati ya wawakilishi wa nchi 57 huko Marekani, pamoja na wajumbe  2,017 kwenye  Baraza la OSCE Huko Austria. 
Kauli mbiu ya Kikao cha Mei 2017 utakuwa ni wanaume na wanawake wote kutoka mashariki na magaharibi katika kujenga mazungumzo ya kidiplomasia, maelewano , ambayo itakauwa ni alama na nguzo na hatua muhimu kuelekea amani , usalama  na ushirikiano.

 

Sr Angela Rwezaula

 Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.